
KLABU ya Simba imeibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya timu ya Polisi Dodoma , mchezo wa kirafiki uliopigwa katika dimba la jamhuri, mjini Dodoma.
Magoli ya Simba yamewekwa kimiyani na Abdi Banda 45+2 akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo, Mwinyi Kazimoto huku goli la pili likifungwa na Said Ndemla akliyepiga shuti kali la umbali w mita 22 na kumshinda mlinda mlango wa Polisi Dodoma dakika ya 60 na mpaka mwamuzi anapuliza filimbi ya mwisho, ubao ulikuwa unasomeka Simba 2-0 Polisi Dodoma.
Mchezo huo ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuunga mkono adhma ya serikali ya kutaka kuhamishia makao makuu ya serikali hiyo mjini Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Tulia Akson alikua mgeni wa heshima kwenye mechi hiyo ambapo aliambatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mh. Nape Nnauye pamoja na viongozi wengine wa serikali ya mkoa wa Dodoma

Simba ilitumia wachezaji wake wengi ambao hawapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo kutokana na wachezaji wengi wa timu hiyo kuitwa kuzitumikia timu zao za taifa. Ibrahim Ajib, Jonas Mkude, Mohamed Hussein, Shiza Kichuya, Muzamiru Yassin wote wapo Nigeria kwenye kikosi cha Stars wakati Laudit Mavugo yeye akiwa kwenye timu yake ya taifa ya Burundi
Post a Comment