
NAHODHA wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi atakosa mchezo wa hatua ya kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 dhidi ya timu ya taifa ya Venezuela baada ya kupata majeraha kweye mchezo wa awali dhidi ya Uruguay.
Messi aliishindia timu yake ya taifa goli walipocheza na timu ya taifa ya Uruguay katika mechi za kufuzu fainali za kombe la dunia kwa jumla ya ushindi wa goli 1-0.
Messi alisema baada ya mchezo huo alipata majeraha na hivyo aliomba kukaa nje kwenye mchezo wa Venezuela utakaopigwa siku ya jumanne.
Kocha wa timu hiyo ya Argentina, Edgardo Bauza alisema, "Ni kweli Messi ameumia na hatuwei kumchezesha kwani hatutaki kumuumiza kwani tunamjali sana" Alisema Bauza.
Baada ya michezo saba kati ya 18, Argentina anaongoza kwa upande wa America Ya Kusini huku akiwaacha Uruguay na Colombia kwa pointi 1.
Post a Comment