SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: RAUNDI YA NNE KOMBE LA EFL MOURINHO, GUARDIOLA USO KWA USO TENA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
DROO ya raundi ya nne ya Kombe la Ligi nchini England maarufu kama EFL Cup imefanyika Usiku wa kuamkia leo ambapo timu mbalimb...






DROO ya raundi ya nne ya Kombe la Ligi nchini England maarufu kama EFL Cup imefanyika Usiku wa kuamkia leo ambapo timu mbalimbali zimewajua wapinzani wao.

Katika droo hiyo imeshuhudiwa mahasimu wawili wa jiji la Manchester yaani Manchester na United wakikutana kwenye mchezo utakaofanyika Oktoba 24.

Hii inakuwa mara ya pili kwa United na City kukutana mara baada ya hapo awali kukutana kwenye mchezo wa Premier League ambapo, Man City walishinda mabao 2-1 kwenye mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Old Trafford.


Katika mchezo huo Manchester United kwa mara nyingine tena watakuwa wenyeji dhidi ya mahasimu wao Manchester City.

Hamu kubwa ya mashabiki wa klabu ya Manchester United ni kuona ni kwa kiasi gani timu yao wangependa ikisawazisha makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa ligi kuu ambao Manchester United walikubali kipigo cha mabao 2-1

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top