
MCHEZAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi
atakuwa nje kwa muda wa majuma matatu baada ya kupata majeraha ya nyonga kwenye
mchezo dhidi ya Atletico Madrid uliochezwa Nou Camp na kumalizika kwa sare ya
bao 1-1 jana.
Nohodha
huyo wa Argentina alipata maumivu hayo punde tu baada ya kumaliza kuwania mpira
na beki wa Atletico Madrid Diego Godin na kuanza kuashiria hali ya maumivu hasa
kwenye upande wake wa kulia.
Jeraha
hilo la Messi inaelezwa awali alipata wakati akiwa na timu yake ya taifa ya
Argentina wiki chache zilizopita, na staa huyo anatarajiwa kuukosa mchezo wa
Champions League dhidi ya Borussia Monchengladbach.
Messi
pia atakosa michezo La Liga dhidi ya timu za Sporting Gijon na Celta Vigo, na
atakuwa hatihati pia kucheza mchezo wa Champions League dhidi ya Manchester
City utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba.
“Kumkosa
Messi maana yake ni pigo katika soka. Tunapokuwa na Messi maana yake tuko
imara, lakini tutajitahidi kuwa imara hata bila ya uwepo wake,” kocha wa
Barcelona Luis Enrique aliwaambia waandishi baada ya mchezo.
Post a Comment