

Mchezo wa Super Cup
umemalizika kwa klabu ya Real Madrid kutwaa kombe hilo kwa ushindi wa goli 3-2
dhidi ya klabu ya Sevilla, timu zote za nchini Hispania.
Mchezo wa Super-Cup
huwakutanisha mshindi wa klabu bingwa barani ulaya ambao kwa msimu wa mwaka
2015-2016 walikuwa klabu ya Real Madrid dhidi ya mshindi wa EUROPA ambao
walikuwa ni Sevilla.
Marco Asensio ndiye
aliyekuwa wa kwanza kuwanyanyua mashabiki wa klabu ya Real Madrid baada ya
kuipatia timu yake bao la uongozi dakika ya 21, goli ambalo lilidumu mpaka
dakika ya 41, Franco Vazquez kuisawazishia Sevila na Yevheniy Konomlyanka
kupachika goli la pili dakika ya 71 kabla ya Segio Ramos kuukwamisha mpira
wavuni na kufanya dakika 90 za mwamuzi kupulizwa, wakiwa wamefungana 2-2
Ilimlazimu mwamuzi wa
mchezo huo kuongeza dakika 30 ambapo ndizo zilikuwa dakika chungu kwa timu ya
Sevila baada ya kukubali kufungwa goli dakika ya 119 na mlinzi wa kulia wa Real
Madrid, Carvajal kuukwamisha mpira wavuni kuipatia Real Madrid goli la ushindi.
Karim Benzema alipaswa
kusubiri mpaka Morata alipotolewa na ndipo alipoingia huku Gareth Bale kuukosa
mchezo huo pamoja na Cristiano Ronaldo nae kuukosa mchezo huo akiwa bado
anaendelea kuuguza jeraha lake alilolipata dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa
katika mchezo wa fainali ya mashindano ya Euro yaliyofanyika nchini Ufaransa.
Post a Comment