SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: RANIERI ANOGEWA NA MAISHA YA KING POWER, AJIFUNGA KITANZI MIAKA MINNE.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  Claudio Ranieri ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu ya Leicester City, mabingwa wa EPL kwa mkataba wa miaka minne. ...


 Claudio Ranieri

Claudio Ranieri ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu ya Leicester City, mabingwa wa EPL kwa mkataba wa miaka minne.

Raineri, 64, raia wa Italia, aliiongoza Leicester, The Fox kutwaa kombe la EPL ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo kuandika historia hiyo huku nayeye Ranieli akitengeneza historia yake.

Ranieri anaungana na wachezaji muhimu wa klabu hiyo Kasper Schmeichel, Wes Morgan na Jamie Vardy ambao pia wameongeza mkataba kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya England.

“Nguvu ambayo ipo hapa, kutoka kwa wamiliki na uongozi kwa ujumla, kwa wachezaji na mashabiki ni jambo zuri sana” Ranieri alisema.

“Msimu ulioisha, ule moyo, pamoja na kujituma kwetu, kulitupelekea kupata mafanikio haya tuliyonayo. Kama tutaendelea kujituma kwa bidii, kuendeleza ile ari yetu na kuendelea kupigana kwa mioyo yetu  sote kwa pamoja, ninaamini tutaendelea kuwa wa mafanikio wote kwa pamoja” Alisema.

Leicester waliopigwa na Manchester United kwenye mchezo wa Ngao Ya Hisani 2-1 siku ya jumapili, watakuwa na kibarua kizito kucheza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi siku ya jumapili, ambapo watasafiri kuwafuata klabu ya Hull City iliyopanda daraja msimu huu.

Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Aiyawatt Srivaddhanaprabha alisema, “Miezi 12 iliyuopita, tulimleta hapa klabuni mtu ambaye tulihisi angetufikisha kwenye hatua nyingine ambayo tulikuwa tunaiwaza muda mrefu. Uwezo wake na kile alichotuzawadia ni zaidi ya hiki tulichokipata” 

Nahodha wa Leicester, Wes Morgan, ambae pia ameongeza mkataba wake mpaka mwaka 2019 amesema, “Kocha ranieri kuongeza mkataba ni habari njema sana, na kuongeza kwamba alikuwa ana msimu bora sana na mafanikio walioyapata msimu uliomalizika, ni furaha ya wote, na vijana wapo tayari kumpa tena sapoti kubwa kuyafikia malengo yake”

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top