SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: JOHN STONES ATUA RASMI ETIHAD.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Klabu ya Manchester City imefabikiwa kunsajili beki wa klabu ya Everton na timu ya taifa ya England, John Stones kwa pauni 47.5mil na k...

Klabu ya Manchester City imefabikiwa kunsajili beki wa klabu ya Everton na timu ya taifa ya England, John Stones kwa pauni 47.5mil na kumfanya kuingia kwenye rekodi ya mabeki walionunuliwa kwa bei ghari duniani.

Stones, 22, raia wa England, amesaini kandarasi ya miaka 6 kuitumikia klabu hiyo ni akiwa mchezaji wa nane kununuliwa na kocha huyo wa matajiri hao wa Manchester, Manchester City wakati wengine wakiwa ni Ikel Gundogun, Gabriel Jesus, Norito, Leroy Sane, Marlos Moreno, Aaron Mooy na Oleksandr Zinchenko.

Stones anaingia kwenye rekodi ya mabeki walionunuliwa kwa gharama Zaidi huku beki wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya PSG David Silver akiwa anashikilia rekodi hiyo ambapo alisajiliwa kwa jumla ya pauni 50mil akitokea klabu ya Chelsea na kujiunga na PSG, mabingwa wa Ufaransa.

Everton waliitolea nje klabu ya Chelsea majira ya joto ya mwaka jana baada ya Chelsea kutoa kitika cha pauni 40mil, na Guardiola akaamua kupanda dau na kuitwaa sahihi ya mchezaji huyo.


‘‘Nafahamu ni vigumu sana kupata nafasi kwenye klabu hii kubwa sana, lakini na mimi ni mtu ninayejitambua,naamini nitafiti kwenye mfumo wa mwalimu kwa haraka zaidi” Alisema mchezaji huyo wa zamani wa Bansley.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top