
KOCHA wa klabu ya mashetani wekundu, Manchester United, Jose Mourinho, amesema suala la uhusiano baina ya wachezaji na mashabiki kwa ujumla, ni jambo la msingi la kuturudisha enzi zile za furaha ndani ya Old Trafford.
Tnagu Sir Alex Fugerson aondoke klabuni hapo, Manchester imekuwa na wastani wa kutwaa pointi 2.02 kwenye mechi za nyumbani ukilinganisha na misimu mitatu iliyopita ambapo kulikuwa na asilimia 2.63.
"Kama tupo uwanja wa nyumbani, halafu mashabiki wa timu pinzani wakatuzidi katika uwezo wa kushangilia zaidi ya mashabiki 70,000, basi itakuwa haina maana hata kidogo, na ina maanisha hatuna ushirikiano" Mourinho alisema.
Mourinho pia amethibitisha kuanza kwa mchezaji wao ghali duniani, Pogba baada ya kuukosa mchezo wa awali, ambao United waliwanyuka AFC Bournamouth kwa jumla ya goli 3-1
Mourinho pia amethibitisha kuendelea kukaa klabuni hapo, mshabuliaji wao toka PSG, Ibrahimovic ambae alisaini kandarasi ya mwaka mmoja pekee.
"Ukitazama uwepo wake unaleta hamasa, na tunaamini ataongeza mwaka tena kuendelea kuwepo kwenye kikosi chetu cha United: Alisema.
Post a Comment