
Wenger amekuwa anakosolewa na mashabiki wa klabu hiyo kwa miaka ya hivi karibuni kwa kuhindwa kufanya usajili wa kikosi hicho licha ya kuwa na namba kubwa ya majeraha.
"Nimetambua tatizo tulilonalo, sasa tunaweza kutumia hela tuliyonao" Wenger alisema.
"NI jambo la muhimu sana kutumia pesa, lakini ni muhimu zaidi kutumia pesa kwa njia inayostahili, Kuna tageti mbili, moja ni kwenye klabu ya hapa England na nyingine ni sehemu yeyote ile" Alisema.
Washika mitutu hao wa London, waliwashuhudia Aaron Ramsey na Alex Iwobi wakitolewa nje baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya EPL dhidi ya Liverpool, walipokubali kichapo cha goli 4-3.
Kikubwa ambacho amekuwa akikisisitiza mzee Wenger, ni kile anachokiita kutumia hela nyingi kwa wachezaji ambao anamini pengine wanaweza wasiwe na msimu bora wakiwa klabuni hapo.
Post a Comment