SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA RWANDA ATIMULIWA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
RWANDA imemtimua kocha wa timu ya taifa Amavubi, Mwingereza Jonathan McKinstry baada ya kushindwa kuiongoza timu hiyo ya taifa kupata m...
McKinstry

RWANDA imemtimua kocha wa timu ya taifa Amavubi, Mwingereza Jonathan McKinstry baada ya kushindwa kuiongoza timu hiyo ya taifa kupata matokeo mazuri.
Taarifa iliyotolewa na wizara ya michezo ya Rwanda imethibitisha kuonyeshwa mlango kwa mkufunzi huyo.
Katibu mkuu wa wizara hiyo kanali Patrice Rugambwa amesema sababu ya kumfuta kazi kocha huyo ni matokeo yasiyo ya kuridhisha ya timu ya taifa Amavubi.
Rwanda kwa sasa ni ya tatu katika kundi lake kuwania tiketi ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Afrika la mataifa nchini Gabon mwakani ikiwa na alama 6.
Kundi hili linaongozwa na Ghana, ikifwatiwa na Msumbiji na Mauritius ya mwisho, lakini haina tena matumaini ya kufuzu.
Jonathan McKinstry alipewa mkataba wa kuifundisha Amavubi mwaka jana na ukarefushwa mwaka huu baada ya kuiwezesha kucheza robo fainali ya mashindano ya CHAN ilipoondolewa na DRC.
Alipoanza kuifundisha timu hiyo ilikuwa katika nafasi ya 68 kwa ubora wa FIFA lakini sasa iko kwenye nafasi ya 121.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top