SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: MANCHESTER UNITED VS SOUTHAMPTON: HII NI ZAIDI YA VITA ZIKUTANAPO TIMU HIZI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
LIGI kuu ya England inaendelea tena leo kwa mchezo kati ya klabu ya Manchester United dhidi ya watakatifu wa Southampton, mchezo ...


Starting XI: <b>Southampton</b> <b>v</b> <b>Manchester</b> <b>United</b> – Barclays Premier ...


LIGI kuu ya England inaendelea tena leo kwa mchezo kati ya klabu ya Manchester United dhidi ya watakatifu wa Southampton, mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Old Trafford kuanzia majira ya saa nne za usiku kwa saa za Africa Mashariki.

 

Kwa United ni mchezo wao wa pili wa EPL ambapo katika mchezo huo, kocha anatarajian kuanzisha kikosi chake kamili ambacho Pogba pia atakuwepo baada ya kuukosa mchezo wa awali kwa kadi ya njano.

Lakini pia, Mourinho anatarajia kumwanzisha Chris Smalling baada ya mechi ya kwanza kukaa nje kwa kadi ya njano uya msimu uliopita.

Kwa upande wa Southampton, nahodha wao Jose Fonte, ambaye amekuwa akihusishwa na mipnago ya kujiunga na United, anaweza kucheza licha ya kuukosa mchezo wa ufunguzi kufuatia kuchelewa kujiunga na wenzake kwenye ‘pre-season’.
Ryan Bertrand atakosekana kutokana na kusumbuliwa na majeraha na nafasi yake itaendelea kuzibwa na Matt Targett.

Meneja wa Southampton Claude Puel, amezungumzia juu ya tetesi za mchezaji wake Jose Fonte kutakiwa na United: 

”Sina tatizo na Jose, ila ni suala la ajabu kidogo kuona tetesi hizi zinakuja wakati tunakabiliana na mchezo dhidi ya United”

“Lakini mbali na hayo ni mchezaji mzuri na amecheza vizuri mazoezini… Jose ana uzoefu, hivyo hawezi kuchanganywa na masuala ya tetesi lakini kinachonishangazwa mimi ni kuona tetesi hizi zinakuja kabla ya mchezo wetu, siku mbili kabla ya mchezo.”

Japo historia haina nafasi katika mpira wa miguu, kuelekea mchezo huo, hii ni tathmini fupi zikutanapo timu hizi.
  • Southampton wameibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye kila mchezo kati ya miwili iliyopita waliyocheza kwenye dimba la Old Trafford.
  • Kabla ya hapo, ndani ya miaka 27 Southampton wamecheza michezo 19 ugenini dhidi ya United bila ya ushindi.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top