SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: ZUNIGA Ajiunga na Watford kwa Mkopo.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Klabu ya Watford ya nchini Wingereza imemsajili beki wa kati wa klabu ya Napoli Juan Camilo Zuniga kwa mkopo lakini akitarajiwa ku...

Juan Camilo Zuniga's challenge on Neymar at the 2014 World Cup ended the Brazil star's tournament


Klabu ya Watford ya nchini Wingereza imemsajili beki wa kati wa klabu ya Napoli Juan Camilo Zuniga kwa mkopo lakini akitarajiwa kuongeza mkataba akifanya vyema.
Zuniga atakayeichezea Watford kwa msimu ujao wakati akitarajiwa ku extend mkataba endapo viongozi wa klabu hiyo kama watavutiwa na huduma yake.
Zuniga anajiunga na aliyekuwa kocha wa zamani wa Napoli msimu wa 2009-2013, aliyesini kuifundisha klabu ya Watford Walter Mazzari.
Zuniga amecheza mechi 62 katika timu ya taifa ya Colombia na alifanikiwa kucheza mara nne katika fainali za kombe la dunia zilizofanyika huko nchini brazil mwaka 2014 na kuwashuhudia timu ya taifa ya Ujerumani kutwaa kombe hilo kwa kuwafunga timu ya Argentina kwa goli moja kwa sifuri.
Zuniga, raia wa Colombia, anaweza kucheza upande wa kulia na kushoto na aliweza kujiunga na Bologna kwa mkopo baada ya kupoteza namba katika kikosi cha Napoli lakini pia kuweza kujiunga na Watford kwa mkopo.
Zuniga 30, anakuwa mtu wan ne kutia kandarasi klabuni hapo huku Mazzari akiwa anaendelea kuhakikisha anatengeneza kikosi bora cha kuweza kupambana ili kuhakikisha wanafanya vyema.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top