SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Tuchel aelezea matumaini katika msimu mpya
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Borussia Dortmund wamewapoteza wachezaji watatu nyota lakini kocha Thomas Tuchel anasema anataraji kuwa na mwanzo mpya na kuwap...




Borussia Dortmund wamewapoteza wachezaji watatu nyota lakini kocha Thomas Tuchel anasema anataraji kuwa na mwanzo mpya na kuwapa wapinzani wao Bayern Munich ushindani mkali katika msimu mpya
Borussia Dortmund walimaliza wa pili katika ligi kuu ya kandanda Ujerumani - Bundesliga na wakafika fainali ya Kombe la Shirikisho la Kandanda Ujerumani - DFB Pokal msimu uliopita lakini kocha Thomas Tuchel anatumai kuwa na mwanzo mpya katika msimu ujao wa Bundesliga wakati kikosi chake kinawakosa wachezaji kadhaa wa zamani nyota.
Tuchel anaendelea na maandalizi ya msimu mpya bila beki Mats Hummels na wachezaji viungo Ilkay Guendogan na Henrikh Mkhitryan, ambao wote wameuzwa.
Lakini Dortmund, baada ya kuwapoteza wachezaji hao, ilijitahidi kuitumia vyema hali hiyo. Klabu ilikusanya zaidi ya euro milioni 100 kutokana na uuzaji wa nyota hao watatu na ikajitosa katika soko la ununuzi wa wachezaji kwa kutumia euro milioni 60.
Beki wa Ureno iliyoshinda Kombe la Ubingwa wa Ulaya 2016, Raphael Guerreiro, beki Marc Bartra, viungo Sebastian Rode, Ousmane Dembele na Mikel Merino, na mshambuliaji Emre Mor wote watajiunga na kikosi hicho wakitaraji kutoa ushindani mkali kwa Bayern ili kuizuia kutwaa taji la tano mfululizo la Bundesliga.

Kikundi cha wachezaji hao waliosajiliwa, ni chipukizi wote na Tuchel anasema anatumai watafanya vyema maana hawakuwa na njia nyingine. Wanaweza kuiga mfano wa Pierre-Emerick Aubameyang na Marco Reus ambao wanafanya vyema katika timu hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top