
Wakati Dortmund wakiendelea kujiimarisha kwa ajili ya msimu mpya, mahasimu wao wakuu Bayern Munich wanaonekana kumrejesha uongozini aliyekuwa rais wa klabu hiyo Uli Hoeness. Baada ya kutumikia kifungo cha miezi 21 jela, Hoeness anarejea katika wadhifa huo, kwa mujibu wa jarida la kandanda la Ujerumani, Kicker.
Hoeness amepewa wadhifa wa heshima wa rais wa klabu, baada ya mkutano wa bodi ya usimamizi, huku mamlaka kamili yakibakia mikononi mwa meneja mkurugenzi Karl-Heinz Rummenigge. Mfanyabiashara na mwanauchumi Karl Hopfner mwenye umri wa miaka 63 amekuwa akishikilia wadhifa huo wa rais wa Bayern Munich tangu Machi 2014 wakati Hoeness alifungwa jela, lakini kila mara alisisitiza kuwa atajiuzulu mara baada ya mtangulizi wake ataondoka jela. Hoeness aliachiwa huru kutoka gereza la Landsberg mwishoni mwa Februari baada ya kuhukumiwa Machi 2014 kwa kukwepa kulipa karibu euro milioni 28.5 za kodi kutoka kwa kampuni yake ya kuuza soseji na nyama.
Bruce amani.
Post a Comment