SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Pride Yaw Owusu: ''Tuliwajua Wachezaji wa Kuwadhibiti"
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Picha na shaffih Kocha wa kikosi cha Medeama Pride Yaw Owusu amesema, walikuwa wanajua wachezaji gani nyota wa Yanga wanaotakiwa kuch...
IMG_0030
Picha na shaffih

Kocha wa kikosi cha Medeama Pride Yaw Owusu amesema, walikuwa wanajua wachezaji gani nyota wa Yanga wanaotakiwa kuchungwa ili kuwadhibiti.
Japo hakuwataja kwa majina ni wachezaji gani ambao walitakiwa kudhibitiwa, Owusu alisema walikuja Dar kwa lengo la kuhakikisha wanashinda mechi dhidi ya Yanga laikini wakashindwa kufanya hivyo.
“Tuliangalia video zao, tuliwajua wachezaji wao hatari na tulijaribu kuwadhibiti. Tulifanya kosa dakika ya kwanza ya mchezo na kilichotokea ni kuruhusu goli la mapema,” alisema kocha huyo ambaye mwaka uliopita alikuwepo kwenye mashindano ya Kagame Cup akiwa kocha msadizi wa Kwesi Appiah wakati wanakinoa kikosi cha Al Khartoum kutoka Sudan.
“Nilikjua mchezo utakuwa mgumu kwetu, kwasababu namfahamu Hans. Tulijaribu kushinda mchezo na hilo ndiyo lilikuwa lengo letu wakati tunakuja hapa lakini alifanya mchezo uwe mgumu.”
“Soka ndivyo ilivyo wakati mwingine unapata matokeo ambayo haukutarajia, tulihitaji kushinda lakini ilikuwa ni vigumu, tulipata nafasi ya wazi dakika za mwisho kumaliza mchezo lakini haikuwa hivyo labda ndivyo ilipangwa iwe hivyo.”
Mchezo mwingine wa kundi A kwenye kombe la shirikisho barabi Africa, utafanyika leo ambapo MO Bejaia watakuwa wanawakaribisha klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo, timu inayoongoza kunfi hilo kwa jumla ya pointi 6.


shaffih

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top