
Pamoja na msimu wa VPL kumalizika tangu mwezi mei, ukiwa ni muda
sasa umepita, leo kumetolewa tuzo za watu waliofanya vizuri na takribani tuzo
kumi na tatu zimeweza kutolewa. Tuzo
zilizokuwa zinagombaniwa ni pamoja na mchezaji bora wa kigeni, iliyokuwa ikiwaniwa
na Donald Mgoma na Thabani Kamusoko wote wa klabu ya yanga pamoja na kipa wa
klabu ya Simba Vicent Agban. Thabani SIkala Kamusoko akaibuka kidedea kwa
kutwaa tuzo hiyo
Zawadi ya mshindi wa nne ilikwenda kwa klabu ya Tanzania
Prisons, wakati mshindi wa tatu akiwa ni Simba na mshindi wa pili akiwa Azam FC
huku mabingwa wa VPL wakiwa ni klanu ya Young Africans wao wakijiita wa
kimataifa.
Zawadi ya mfungaji bora ilikwenda kwa mchezaji wa kigeni
anayekipiga klabu ya Young African kutoka nchini Burundi AmisiTambe aliyefunga
magoli 21 mbele ya Hamis Kiiza aliyekuwa na magoli 19.
Kocha bora wa msimu alikuwa nim kocha wa klabu ya Young
Arican Hans Van Pluijm aliyewapiku wenzake wote na kutwaa tuzo hiyo ikiwa ni
mara yake ya kwanza.
Tuzo ya goli bora ilikuwa inawaniwa na Amis Tambwe pamoja na
Ibrahim Ajib Migomba wa Simba aliyekuwa na magoli mawili na Migomba kuibuka na
tuzo hiyo kwa goli alilolipata wakati walipocheza na klabu ya Mgambo JKT.

Tuzo ya mcheza bora wa mwaka ilikuwa ipambanishwa na akina Shiza Kichuya aliyekuwa mtibwa na kuweza
kusajiliwa na klabu ya Simba, Juma Abdul Mnyamani pamoja na Muhamed Hussein na
Tuzo hiyo kuchukuliwa na Juma Abdul Mnyamani.
Tuzo nyingine zilizotolewa usiku huu ni pamoja na mwamuzi
bora iliyochukuliwa na Ngole Mwangole, Timu yenye nidhamu wakati Mtibwa Sugar
wakinyanyua tuzo hiyo huku tuzo nyingine ni ile ya mchezaji bora chipukizi
iliyochukuliwa na mchezaji wa Simba Muhamed Hussein Zimbwe Junior huku kipa
bora akiiubaki Aishi Manulla wa klabu ya Azam fc
Kwa mahesabu ya haraka haraka, kati ya tuzo 13 zilizokuwa zinagawiwa, tuzo 5 zimechukuliwa na klabu ya yanga tuzo hizo zikiwa ni kocha bora, mchezaji bora, mfungaji bora, mchezaji bora wa kigeni pamoja na timu kuchukua ubingwa.
Post a Comment