Raia huyo wa Senegal
mwenye umri wa miaka 31 alikabiliwa na mlinzi wa timu hasimu katika ligi kuu ya
Uchina hapo jana Jumapili tarehe 17 Julai.
Ba ambaye anaichezea
Shanghai Shenhua aligongwa na mchezaji wa timu hasimu ya Shanghai SIPG mita
chache tu kabla ya kisanduku cha hatua 18, Alipoanguka mguu wake ulipinduka kwa
hali isiyo ya kawaida na kuvunjika papo hapo.
Video ya mechi hiyo
inaogofya haswa inavyoonesha wazi wazi mguu wake umevunjika kati ya goti na
kisigono.
Kocha wa klabu yake
Gregorio Manzano ameonya kuwa tukio hilo linaweza kumlazimisha nyota huyo
kustaafu kucheza soka .
Ba
aliwahi kuichezea West Ham, Newcastle na Chelsea zote katika ligi kuu ya
Uingereza kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya Uchina akitokea Uturuki katika
klabu ya Besiktas.
Uhamisho huo yamkini
uligharimu takriban pauni milioni 12.
Msimu huu Ba anaongoza
orodha ya wafungaji mabao akiwa na jumla ya mabao 14 katika mechi 18
alizoshiriki.
Post a Comment