
.
Ronaldinho Gaucho amesema, Lionel Messi
bado ni mchezaji bora duniani licha ya kushindwa kuipatia timu yake ya taifa ya
Argentina mataji makubwa duniani.
Messi 29, ni mfungaji bora katika nchi
yake akiwa ameifungia Argentina magoli 55, amestaafu kucheza kimataifa mwezi uliopita
baada ya kukubali kupoteza fainali ya Copa Amerika dhidi ya timu ya taifa ya
Chile kwa miaka miwili mfululizo.
Messi ambae ameshinda taji la Ballon d'Or mara tano, amecheza fainali ya
Copa America mara tatu na fainali ya kombe la dunia mwaka 2014 na kuweza
kupoteza mataji yote.
Cristiano
Ronaldo hivi karibuni ameshinda kombe la EURO akiwa na timu yake ya taifa ya
Ureno, na hivyo kuibua mjadala mzito ya kwamba kati yao wote wawili, ni nani
mchezaji bora Zaidi ya mwenzake lakini Ronaldinho ambae alifanikiwa kushinda
kombe la dunia mwaka 2002 na timu ya Brazil, anaamini kwamba Messi aliyekuwa
mchezaji mwenzake wakati wapo timu ya Barcelona ni bora Zaidi.
‘‘Kwangu
mimi, Messi kustaafu soka kimataifa, haibadilishi kitu” Gaucho alisema.
‘‘Bado
ni mchezaji bora wa dunia, heshima niliyonayo kwake, haibadiliki kamwe” ‘‘Na
kama kweli ameamua kustaafu kuichezea timu ya taifa, basi wanamichezo watakosa
uwepo wake na mashabiki kwa ujumla”
Ronaldinho
Gaucho aliyewahi kushinda tuzo ya Ballon
d'Or mwaka 2005, kipindi cha miaka mitano kabla ya kuachiwa na
Barcelina, amesema alikuwa anamlea Messi wakati wanacheza wote Nou camp na anaamini
ya kuwa Mwargentina huyu amekuwa ni mwongozo kwa akina Neymer kwa kipindi chote
na kuisadia timu yao kutwaa mataji.
‘‘Japo
nipo mbali nisiweze kuona kinachoendelea klabuni hapo, lakini mwangozo na
ujumbe niliokuwa nao mimi kwa Messi, ndio kitu hicho hicho anachokifanya Messi
kwa Neymer kwa sababu ni muhimu sana kwa mchezaji mzoefu kushare vitu tofauti
na wachezaji wachanga” Gaucho alifafanua.

Na
Gaucho akamalizia akisema, ‘‘NA hicho ndicho kitu kikubwa sana kilichompelekea
Neymer kuzoea mfumo wa Barcelona na kufiti kama walivyokuwa yeye [Gaucho] na
Messi.
Huo
ni mtazamo wa aliyekuwa mchezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona ya nchini
Hispania, akiwa anaamini bado Ronaldo si kitu mbele ya Messi alivyokuwa
akihojiwa na skyspot. Wewe mtazamo wako uko wapi kati ya hawa mabwana wawili,
Ronaldo anastahili kuitwa mchezaji wa dunia, kama ni ndio, unathibitisha jibu
lako kwa vigezo gani, na kama ni kinyume na hayo, pia unatumia vigezo gani?
Post a Comment