
Jose Mourinho kwa mara ya kwanza jana alisimama kama kocha wa
Manchester United kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Wigan Wigan Athletic na
kushuhudia timu yake ikipata ushindi wa mabao 2-0, magoli yaliyofungwa na Will
Keane na Andreas Pereira.
Haya ndio mambo kadhaa makubwa yalioonekana kutokana na mchezo wa
jana.
Aina yake ya Staili ya uchezaji imeanza kuonekana
Licha ya kwamba huo ndio ulikuwa mchezo wa kwanza kama kocha wa
Manchester United, lakini tayari kumeokana viashiria vya aina yake ya mchezo
katika timu hiyo. Walikuwa wanamiliki mpira kidogo huku wakitumia mfumo wa
4-2-3-1 ambao pia ulikuwa ukitumiwa na kocha wa zamani wa klabu hiyo Louis van
Gaal lakini utofauti ulikuwepo kwenye pesi ya mchezo. Jana mchezo ulikuwa
kwenye tempo ya hali ya juu. Wachezaji walikuwa na uhuru mwingi lakini vile
vile aina ya mashambulizi yalikuwa ni ya moja kwa moja, na pia baadhi ya
wachezaji walionekana kuwa nguvu kubwa kama Ander Herrera.
Baada ya mchezo Mourinho mwenyewe alionekana kuanza kuwakubali
wachezaji wake na kusema kwamba wachezaji wanaonesha kuelewa anachowaelekeza.

Henrikh Mkhitaryan anaweza kuchezeshwa namba 10 ya kudumu
Watu wengi walikuwa wakitupia macho kwa wachezaji wapya hasa
Henrikh Mkhitaryan. Licha ya kukosa goli la wazi lakini alionekana kuonesha
uwezo wa hali ya juu. Mipira yake mingi ilionekana kuwa na hatari, alikuwa akizunguka
sehemu zote za uwanjakulia, kushoto na katikati. Ikumbukwe huyu ndiyo mchezaji
aliyeongoza kwa kupiga pasi nyingi za mabao msimu uliopita kwenye ligi ya
Bundesliga wakati akicheza Borussia Dortmund.
Luke Shaw anaonekana kumvutia bosi wake mpya.
Baada ya kukaa nje kwa miezi 10 kutokana na jeraha la mguu, Luke
Shaw alionekana kutokuwa na woga na kupandisha timu wakati akicheza beki ya
kulia.
Zaidi ya hapo Mourinho alimsifu sana baada ya kuamua kuahirisha
kwenda mapumzikoni na kuamua kufanya mazoezi kwa bidii ili kurejea katika ubora
wake wa awali baada ya kukaa nje kwa muda mrefu.
Juan Mata alikuwa na mchango mkubwa licha kuingia kipindi cha
pili japo si kipaumbele cha Morinho.
Katika kikosi cha kwanza kilichotajwa katika mchezo dhidi ya
Wigan hapo jana, jina la Mata halikuwepo na kwamba Mourinho alimuanzisha
benchi. Katika mabadiliko aliyofanya kipindi cha pili, Mourinho alimuingiza
Mata na kutoa pasi ya goli la kwanza lililofungwa na Will Keane baada ya
kuunasa kwa umaridadi wa hali ya juu mpira uliokuwa ukipigwa na kipa wa Wigan
kwenda kwa beki wake.

Hiyo ilikuwa ni mechi yake ya kwanza ya Jose Morinho akiwa
anaifundisha klabu ya Manchester United na mashabiki wa klabu hiyo wakitarajiwa
makubwa kutoka kwake msimu utakaoanza agosti.
Wakati mashetani wekundu wakishangilia ubora wa kikosi chao,
mahasimu wao wa upande wa pili klabu ya Chelsea inayofundishwa na mkunfunzi
Antonio Conte raia wa Italia imekubali kichapo cha goli 2-0 na klabu ya Rapid
Vienna, mchezo ukiwa ni wa kirafiki katika maandalizi ya msimu ujao.
Post a Comment