
Kampuni ya mashindano ya bahati nasibu inayodhamini Ligi Kuu ya Kenya
imetia saini mkataba wa kuwa mdhamini wa klabu ya Hull City ya Uingereza.
Kampuni hiyo ya SportPesa, ambayo huandaa mashindano ya
kubashiri matokeo ya mechi nchini Kenya, imetia saini mkataba wa kudhamini Hull
City kwa misimu mitatu.
Klabu ya Hull City ilifanikiwa kurejea kwenye Ligi ya Premia msimu
utakaoanza mwezi ujao.
Hull City watafungua msimu kwa mechi ya nyumbani dhidi ya
mabingwa Leicester City.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa klabu hiyo, udhamini wa
SportPesa ndio wa juu zaidi kuwahi kupokelewa na klabu hiyo katika historia
yake ya miaka 112.
Hull City imekuwa ikidhaminiwa na kituo cha burudani cha
Flamingo Land.
Post a Comment