
Arsenal wanahitaji kufanya usajili zaidi kutokana na kukosa
wachezaji wenye ubora wa juu huku Mesut Ozil, Alexis Sanchez na Granit Xhaka
wakisemwa kwamba si wazuri kwa kiwango hicho, hii ni kwa mujibu wa Stan
Collymore.
Arsene Wenger amemsajili Xhaka pamoja na Takuma Asano kwenye
dirisha hili la usajili huku akisisitiza kwamba yuko tayari kutumia pesa
kusajili isipokuwa kwa wachezaji sahihi tu kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Arsenal tayari wamewakosa Jamie Vardy huku Gonzalo Higuain
akitajwa kuwa njiani kujiunga na Juventus, na hivyo basi, Collymore anahisi
kwamba kuna uhitaji mkubwa wa klabu hiyo kufanya usajili wa maana zaidi ili
kuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa kwenye mbio za kuwania taji la ligi la msimu
ujao.
“Bado naamini kwamba timu hii ya Wenger itakuwa katika nafasi
nne za juu endapo tu watasajili beki wa kati mzuri na mshambuliaji wa kati
mzuri, vinginevyo sidhani kama watakuwa na fursa hiyo,” ameandika kwenye gazeti
la Sunday Mirror.
“Kwamba, kwa timu ambayo mawazo yake makubwa ni kupata nafasi ya
kushiriki Michuano ya Uefa kila msimu, hii litakuwa ni janga kubwa.
“Ni ukweli ulio wazi kwamba timu ya Wenger ina huo uhitaji,
lakini bado anaonekana kuwa mbishi kutumia fedha ambazo hata hivyo si zake,
unaweza kuona kwamba wakati wa Arsenal ya Sol Campbell, ukuta ulikuwa
hauoenyeki kirahisi.
“Vile vile bado sioni kama Mesut Ozil, Alexis Sanchez au Granit
Xhaka ni wachezaji wa viwango vya juu kiasi hicho. Kweli ni wachezaji wazuri.
Xhaka ni usajili sahihi, ni mchezaji ambaye ni katili uwanjani lakini vile vile
ananyumbulika.
“Lakini hata hivyo usajili huu hauna maana kwamba Arsenal ndio
wamemaliza kama ambavyowenzao wamemleta mtu kama Zlatan Ibrahimovic na sasa
mbioni kuleta mtu kama Paul Pogba.
“Kama Wenger angemleta Suarez wakati ule, sasa angekuwa anapiga
goli za kutisha kuliko hata anavyofanya kunako klabu ya Barcelona,” amemaliza.
Post a Comment