Udhamini
huo umetolewa na shirika la hifadhi za taifa (Tanapa) kupitia kwa mkurugenzi
mkuu wa shirika hilo na kukabidhiwa kwa wachezaji hao.
Ufadhili
huu unalengo kuisadia timu ya taifa na kuwezesha kufanya vizuri katika michuano
ya Olimpiki na pia kusaidia kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania.
Baada
ya kupata ufadhili huo .Rais wa shirikisho la riadha nchini Antony Mtaka
amesema fedha hizo zitatumika kulipia kadi za bima ya afya ya wachezaji hao na
familia zao kwa muda wa mwaka mmoja.
Akizungumza
kwa niaba ya wachezaji hao, Alfonce Felix amesema ufadhili huo utawaongezea
chachu ya ushindi na kuitangaza nchi.
Timu
hiyo ya riadha yenye wachezaji wanne inaendelea na maandalizi ya mwisho chini
ya kocha wake Francis John katika kambi yake ya West Kilimanjaro mkoani
Kilimanjaro.
Post a Comment