SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: DABI YA JIJINI MANCHESTER NI ZAIDI YA DABI YA MORINHO NA GUARDIOLA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ligi kuu ya EPL kwa msimu utakaoanza mnamo tarehe 13 ya mwezi ujao, kuna sura kadha wa kadha ambazo si ngeni sana machoni pa wapenda soka...
Ligi kuu ya EPL kwa msimu utakaoanza mnamo tarehe 13 ya mwezi ujao, kuna sura kadha wa kadha ambazo si ngeni sana machoni pa wapenda soka, lakini pengine ugeni utajitokeza pale katika ligi hiyo maarufu sana duniani. Sura za akina Morinho zimekwisha zoeleka kwani kocha huyo maarufu sana ulimwenguni alikwishawahi kufanya kazi na klabu ya Chelsea pamoja na Real Madrid ya nchini Hispania lakini pia hata ule wakati anachukua kombe la klabu bingwa barani ulaya akiwa na klabu ya Inter ya nchini Italia.

Tuachane na hayo, mahasimu wawili Pep Guardiola pamoja na Jose Morinho watakuwa wakivinoa vilabu vya jijini Manchster, Morinho akiwa kwa mashetani wekundu wakati Guardiola atakuwa upande wa pili wa shilingi akikinoa klabu cha Manchster City vyote vikiwa katika mji mmoja na waswahili wengi huvitofautisha kwa kuvipa majina ya MU ni ya kijijin wakati M/city ni ya mjini.
Siku zikutanapo timu hizi katika ligi kuu huwa ni DABI iliyobeba hisia mbalimbali haswa kwa kila nafasi ya klabu moja moja lakini pia hata historia ya timu hizo kubwa sana duniani.

Mwaka huu, utamu wa mechi hiyo unanogeshwa Zaidi na uwepo wa hawa makocha wakubwa na historia zao Guardiola pamoja na Morinho na hivyo DABI kuhama toka kwenye timu mpaka kwa wakufunzi. Nani Zaidi ya mwenzake, ni swali ambalo mimi na wewe, tutakosa majibu mazuri sana ya ushawishi kwa watu Zaidi ya kusema tukae na tusubiri mpaka wakati mwafaka tutakapoona picha halisi ya kila kocha na nafasi ya timu yake.

Mara ya mwisho Pep Guardiola na Jose Morinho kusalimiana kwa kushikana mikono ni kile kipindi wakati Guardiola akiifundisha klabu ya Barcelona wakati Morinho akiwafundisha mahasimu wao wakubwa klabu ya Real Madrid kile kipindi kuanzia mwaka 2010-2012 kabla ya kila mmoja hajatimkia kwake.

 Hii ni Zaidi ya DABI ya jiji la Manchester wanapokutana mafahari hawa wawili na kipimo kikubwa kinaanza hapo siku ya kesho watakapokutana katika michezo ya kujiandaa na msimu ujao inayofanyika huko nchini China.

Manchester United wanakutana na Manchester city huku Morinho akiwa amejeruhiwa vilivyo na klabu ya BVB ya nchini Ujerumani kwa magoli 4-1 mchezo uliofanyika siku ya alhamisi.

Kuelekea mchezo wa hiyo leo, kila kocha ameonyesha kutokuwa na hofu na kocha mwenzake na haya aliyaongea Morinho wakati walipotua njiani baada ya ndege yao kukutana na anga iliyokuwa haijatulia na hivyo kuweza kuahirisha safari yao kuelekea mji wa Shanghai.

Kwa upande wa shilingi, nae Guardiola ameonyesha kutokuwa na uadui na kuweza kuthibitisha ya kuwa Morinho ni rafiki yake mkubwa na walisha wahi kufanya kazi nae sehemu moja, kwahiyo kumsalimia kwa kumpa mkono kwake wala sio zoezi gumu kiasi hicho walichokuwa wanakifikiri waandishi wengi wa habari za michezo.

Safari ni ndefu wakati Morinho ni sawa na fisi aliyepewa mfupa mzito kuutafuna na wakati huo hajala siku nzima, kwake ni zoezi ambalo pengine linaweza kuwa tatizo kubwa sana wakati Guardiola atahitaji uvumilivu wa hali ya juu kutoka kwa mashabiki wa M/city ili kuweza kupandikiza falsafa zake kuliko kushikiwa bango kutaka matokeo ya haraka.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top