
Pamoja ya kutolewa nje
mapema kwenye mchezo wa fainali, nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo ameongeza
kitu kingine kwenye maisha yake ya soka.
Akicheza kwa mara ya
nne kwenye michuano ya Ulaya, mwisho wa siku nyota huyo mwenye miaka 31
alinyanyua ndoo kutokana na ushindi wa kikosi wa bao 1-0 katika dakika za
nyongeza kwenye dimba la Stade de France dhidi ya wenyeji Ufaransa. Ilikuwa ni
kumbukumbu nyingine kwa star huyo wa Real Madrid ambaye amekuwa akifanya vizuri
kwenye michuano ya Ulaya tangu alipoanza kucheza kwa mara ya kwanza mwaka
2004 akiwa na umri wa miaka 19.
Ameweza kuifikia
rekodi ya mfungaji wa muda wote Michel Platini kwa kufunga magoli matatu katika
fainali za mwaka huu baada ya kufunga goli kwa kichwa kwenye mechi dhidi ya
Wales. Pamoja na magoli mawili dhidi ya timu ya taifa ya Hungary na hivyo
kuifika rekodi aliyokuwa anaishikilia mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya
Ufaransa Michel Plattin kwa jumla ya magoli 9. Kwa idadi hiyo sasa Ronaldo
anaweka rekodi ya kuwa na magoli mengi katika mashindano ya mataifa ya ulaya
pamoja na Plattin kwa jumla ya magoli 8 huku akifuatia na akina Alan Shearer
raia wa Wingereza akiwa na magoli 7.
Ronal alisafiri
kuelekea Ufaransa akiwa ameshacheza mechi 14 katika fainali mbalimbali
zilizopita. Siku chache baadaye akaivunja rekodi ya golikipa wa Uholanzi Edwin
van der Sar na beki wa Ufaransa Lilian Thuram ya kucheza mechi 17 kwenye sare
ya magoli 3-3 dhidi ya Hungary. Akianza kwenye mchezo wa fainali dhidi ya
Ufaransa sasa ameweka rekodi ya kucheza mechi 21 kwenye michuano hiyo.
Licha ya kwamba
alikosa mkwaju wa penati kwenye mchezo kati ya Ureno dhidi ya Austria, mchezaji
huyo wa zamani wa Sporting CP na Manchester United amevunja rekodi ya star
mwingine wa Ureno Luis Figo ya kucheza mechi nyingi kwenye kikosi cha Ureno kwa
kufikisha mechi 128 huku LuÃs Figo akiwa amecheza mechi 127 katika miaka ya
1991-2006.
Mchezaji wa kwanza kufunga kwenye Euro nne tofauti, Ronaldo alianza michuano ya Euro 2016 akiwa
miongoni mwa wachezaji saba ambao wameshafunga katika mara tatu katika Euro
tatu tofauti na alikuwa akipambana na Zlatan Ibrahimović kuwa mchezaji wa
kwanza kuweka rekodi ya kufunga kwa mara ya nne katika Euro nne tofauti.
Alisubiri hadi mechi
ya tatu kuweza kukamilisha hilo katika michuano iliyomalizika nchini Ufaransa
lakini mpinzani wake msweden Zlatan hakuweza kufumania nyavu. Ronaldo aliweka
rekodi hiyo baada ya kupiga bao mbili kwenye mechi dhidi ya Hungary. Alipofunga
goli kwenye mchezo dhidi ya Wales akawa mchezaji wa kwanza kufunga magoli
matatu katika fainali tofauti za Euro.
Mfungaji bora wa muda wote wa Euro (mechi za kuwania kufuzu zimehesabiwa)
Nyota huyo wa Ureno
anamuongoza Ibrahimović kwenye orodha ya mfungaji wa muda wote kwenye michuano
ya Euro ukichukua magoli yake tisa aliyofunga kwenye fainali za michuano hiyo
ukijumlisha na magoli mengine 20 aliyofunga kwenye mechi za kuwania kufuzu,
matano kati ya hayo amefunga wakati wa kuwania kufuzu kucheza fainali za mwaka
huu zilizofanyika Ufaransa na kuwa na jumla ya magoli 29.
Kwa upande mwingine, rekodi mbili za Ronaldo zilivunjwa kwenye michuano
iliyomalizika…
Mchezaji mwenye umri
mdogo kucheza fainali ya Eurok Fainali ya Jumapili ilikuwa ni ya pili kwa
Ronaldo baada ya kuandika historia kwenye fainali yake ya kwanza ya Euro mwaka
2004.
Mechi hiyo ya mwaka
2004 ilimalizika kwa Ureno kufungwa na Ugiriki lakini Ronaldo aliacha alama ya
kuwa mchezaji mwenye miaka 19 na siku 150 kucheza fainali ya Euro rekodi ambayo
ilidumu hadi ilipovunjwa na Renato Sanchez aliyeanza kwenye kikosi cha Ureno
kilichocheza fainali dhidi ya Ufaransa akiwa na miaka 18 na siku 328.
Ronaldo pia alikuwa
mchezaji mdogo kwenye michuano mikubwa alipokuwa kwenye kikosi cha Ureno
kilichoshiriki fainali za Euro mwaka 2004 na kufunga goli kwenye mchezo
waliochapwa 2-1 na Ugiriki kwenye mchezo wa ufunguzi akiwa na miaka 19 na siku
128. Renato Sanches akajaingia akitoka benchi kwenye mchezo wa kwanza kwenye
fainali za mwaka huu akiwa na miaka 18 na siku 301 na kuvunja rekodi ya Ronaldo
kwenye mechi waliyobanwa na kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Iceland.

Timu ya taifa (Ureno) kwa ujumla.
·
Mchezaji aliyecheza
mechi nyingi kwenye michuano ya Euro: 21
·
Mchezaji mwenye magoli
mengi kwenye fainali za Euro: magoli 9 (sawa na Michel Platini)
·
Mchezaji aliyefunga
kwenye michuano mingi ya Euro: Euro 4
·
Mchezaji pekee kufunga
magoli matatu kwenye fainali mbili za Euro
·
Magoli mengi kwenye
michuano ya Euro ukijumlisha na ya kuwania kufuzu: magoli 29
·
Mechi nyingi kwenye
kikosi cha Ureno: 133
·
Mfungaji mwenye magoli
mengi kwenye timu ya Ureno: 61
Post a Comment