SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Kutoka Best Loser Mpaka kuwa Bingwa.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kutoka Best Loser Mpaka kuwa Bingwa. Mashindano ya UEFA EURO 2016 yamehitimishwa leo kwa mchezo wa fainali kati ya wenyeji wa mashind...
Kutoka Best Loser Mpaka kuwa Bingwa.






Mashindano ya UEFA EURO 2016 yamehitimishwa leo kwa mchezo wa fainali kati ya wenyeji wa mashindano hayo, Timu ya taifa ya Ufaransa walipokubali kichapo cha goli moja kwa nunge toka timu ya taifa ya Ureno.
Dakika 90 zimemalizika kwa sare tasa na hivyo refa kuongeza dakika 30, na katika dakika ya 109 Eder akawa amekamilisha safari ya timu ya taifa ya Ureno baada ya kuupachika mpira nyavuni akiupiga nje ya box na kuiandikia Ureno historia mpya.
Ureno iliyokuwa na msimu mbovu tangu kuanza kwa mashindano na kumaliza katika hatua ya makundi akiwa wa tatu na kuchukuliwa kama best loser, ameweza kuzinduka katika dakika za mwishoni na kuyafanya maajabu ambayo watu bado kama wanaamini ya kuwa huenda wakawa wanaota kumbe ni kweli tukio limekwisha tokea.
Kwa ureno inakuwa ni mara ya kwanza kubeba kombe la mataifa ya ukaya, wakati wapinzani wao, Timu ya taifa ya ufaransa wakiwa wamechukua mara 2 mwaka 1984 na mwaka 2000.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top