
Liverpool
wamefanikiwa kumnasa beki Ragnar Klavan kutoka klabu ya Augsburg ya Ujerumani
kwa mkataba wa miaka mitatu.
Klavan (30) ambaye amesajiliwa na ada ya paundi milioni
4.2 ataungana na wenzake Jumanne ijayo nchini Marekani ambapo wameweka kambi
kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi.
Beki huyo mwenye uzoefu mkubwa amesajiliwa kwa jili ya
kusaidiana na Mamadou Sakho na Joe Gomez ambao kwa sasa wanasumbuliwa na
majeraha
Atakuwa akivaa jezi namba 17 ambayo awali ilikuwa
ikivaliwa na Sakho
Nahodha huyo wa Estonia anakuwa mchezaji wa tano
kusajiliwa na Liverpool msimu huu huku akiwa ni mchezaji wa tatu kusajiliwa kutoka
Bundesliga chini ya utawala wa Klopp.
Post a Comment