
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61, ambaye
amekuwa akikinoa kikosi hicho toka Septemba mwaka 2014, aliiongoza Ureno kutwaa
taji lake la kwanza kubwa la kimataifa pamoja na kucheza bila nyota wake
Cristiano Ronaldo katika fainali dhidi ya wenyeji Ufaransa mapema mwezi huu.
Mkataba wake mpya alioongezwa utamfanya
kukiongoza kikosi hicho katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na ile ya
mataifa ya Ulaya. Timu ya taifa ya Ureno itaanza kampeni zake katika harakati
za kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 za huko Urusi na timu ya
taifa ya Switzerland
tarehe 6 septemba.
Santos
amewahi kufundisha klabu kubwa nchini Ureno zikiwemo Benfica, Sporting Lisbon
na Porto huku pia akiwahi kuinoa timu ya taifa ya Ugiriki.
Post a Comment