
Hatimaye
mikakati ya kupunguza tabia zisizovumilika kwa wachezaji na mameneja katika
soka la Uingereza umetangwazwa rasmi Katika taarifa iliyotolewa na Chama cha
Soka cha nchi hiyo imedai kuwa maadili mabovu yamefikia hatua ya kutokubalika.
Kuanzia msimu huu mpya wa ligi, kadi
nyekundu zitaonyeshwa kwa mchezaji atakayemfuata mwamuzi wa mchezo na kutumia
lugha isiyokuwa sahihi au kumuonyesha ishara yeyote mbaya.
Tabia katika maeneo ya benchi la
ufundi pia nazo zitachukuliwa hatua kali. Mwenyekiti wa Ligi Kuu Richard
Scudamore amesema kumekuwa na wasiwasi kwa kipindi kirefu kuwa wachezaji
wamekuwa wakivuka mipaka kwa tabia zao wanazoonyesha. Makosa ambayo mchezaji
anaweza kupewa kadi ya njano, Kuonyesha wazi kutomuheshimu mwamuzi wa mchezo.
Kuonyesha shari kwa maamuzi
yaliyotolewa, Kumvaa mwamuzi uso kwa uso ,Kumkimbilia mwamuzi ili kupinga
uamuzi uliotolewa Shambulizi, lugha ya matusi au ya kunyapaa na ishara yeyote
kumuelekea mwamuzi, Kugusana na mwamuzi yeyote katika tukio ambalo sio la
kumfanyia fujo ,kadi ya njano walau kwa mchezaji mmoja wakati wachezaji wawili
au zaidi, watakaoenda kumzonga mwamuzi.
Makosa mapya ambayo mchezaji anaweza
kupata kadi nyekundu ni, Kama mchezaji atamvamia mwamuzi na kumshambulia,
kutumia lugha ya matusi au kunyanyapaa au kumnyooshea ishara kwenda kwake, Kugusana
na mwamuzi wa mchezo kwa nia ya kumfanyia fujo au kupingana na uamuzi wake.
Post a Comment