SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: PAUL LE GUEN AMEONGEZWA KATIKA BENCHI LA UFUNDI LA SUPER EAGLES.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Paul le Guen ameteuliwa kuwa kama mshauri wa benchi mpya wa timu ya taifa ya Nigeria kufanya kazi pamoja na meneja Salisu Yusuf, ambae ...





Paul le Guen ameteuliwa kuwa kama mshauri wa benchi mpya wa timu ya taifa ya Nigeria kufanya kazi pamoja na meneja Salisu Yusuf, ambae atakuwa kocha mkuu. Mfaransa huyo mwenye miaka 52 amewahi kuwa mkufunzi wa Lyon, PSGpamoja na Rangers na kuweza kuiongoza timu ya taifa ya Cameroon kufuzu fainali ya kombe la dunia ya mwaka 2010 iliyofanyika ardhi ya Africa kwa mara ya kwanza.
Uteuzi wa Le Guen na mkataba wake, ni suala la makubaliano, yeye na shirikisho la mpira wa miguu la Nigeria NFF
Sundey Oliseh alikuwa kocha wa Sundey Oliseh alikuwa kocha wa kudumu wa mwisho wa Super Eagles kabla ya yeye kujiondoa mwezi Februari katika mkataba wake.
Kocha Imama Amapakabo na mkufunzi wa makipa Alloy Agu, watakuwa pamoja na Le Guen na Yusuf, ambaye alikuwa msimamizi wa Super Eagles waliposhinda mechi za kirafiki dhidi ya Mali na Luxembourg mwezi Mei. Nigeria wameshindwa kufuzu fainali za  kombe la mataifa ya Africa za  2017, nchini Gabon, lakini wapo kwenye raundi ya mwisho ya michezo ya kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 zitakazofanyika huko nchini Urusi
Nigeria wametolewa  katika Kundi B, wakiwa na vinara wa Afrika kwa ubora wa viwango vya FIFA, timu ya taifa ya Algeria, lakini pia Cameroon pamoja na Zambia. 
Kamati ya benchi la ufundi la NFF ilipendekeza kwamba kocha msaidizi wa zamani wa Super Eagles, Bitrus Bewarang atapewa jukumu la ukurugenzi katika timu ya taifa ya Nigeria. 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top