SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Mtibwa Sugar, Mbeya City Kucheza Mechi Ya Kirafiki.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ikiwa ni wakati maridhawa kwa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara kijifua kabla ya msimu mpya kuanza, Timu kadha wa kadha zi...
IMG-20160719-WA0035


Ikiwa ni wakati maridhawa kwa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara kijifua kabla ya msimu mpya kuanza, Timu kadha wa kadha zimekuwa zikitafuta maeneo tulivu kwaajili ya kuweza kuvinoa vilabu vyao kabla ya kuanza rasmi kwa msimu mpya wa 2016-2017 unaotarajiwa kuanza rasmi tarehe 20 ya mwezi Agosti.
Wakati hayo yakiendelea, Vilabu viwili, Mbeya city na Mtinwa sugar vimekubaliana kucheza mchezo wa kirafiki utakaofamyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Morogoro tarehe 30 ya mwezi huu, jumamosi ya mwisho ya mwezi wa saba.
Taarifa kutoka uongozi wa Mbeya City pamoja na ule wa Mtibwa Sugar  inasema, Kwa mujibu wa kiongozi wa Kanisa la Faith Baptist, Mch Jerry Wyatt ambaye ndiye mwandaaji na msimamizi mkuu wa mchezo huo, amesema maandalizi yote ya mechi hiyo ya kirafiki itakayoambatana na tamasha kubwa la mahubiri ya neno la Mungu tayari yamekamilika ikiwa ni pamoja na timu zote kuthibitisha kuhudhuria.
‘‘Maandalizi yote yamekamilika, timu zote zimethibitisha kushiriki katika mchezo huo ambao utaambana na mahubiri ya neno la Mungu kwenye uwanja wa Jamhuri, naomba watu wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia mchezo mzuri wa kirafiki kutoka kwa timu hizi mbili pia kupata mahubiri mazuri ya neno la Mungu pasipo kiingilio chochote kwa watakaofika kwenye uwanja wa Jamhuri”
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Mtibwa sugar na Mbeya City kucheza mchezo wa kirafiki ulioandaliwa na Kanisa hilo awali ikiwa ni msimu uliopia ambapo timu hiyo kutoka Manungu iliibuka na ushindai wa bao 1-0 lililofungwa kipindi cha pili na Mohamed Ibrahim
City inatarajia kuondoka Mbeya Julai 28 tayari kwa mchezo huo uliopangwa kupigwa siku jumamosi ya mwisho wa mwezi huu.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top