
Golikipia wa klabu ya Liverpool Loris Karius raia wa Ujerumani, anatazamiwa kukaa nje kwa majuma kumi baada ya kuvunjika mkono kwenye mechi yao ya kirafiki walipokubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya klabu ya Chelsea ya huko nchini England katika mwendelezo wa mechi za kirafiki.
Karius 23, aliyejiunga na klabu ya Liverpool kwa kitita cha pauni 4.7mil akitokea klabu ya Meinz ya Ujerumani, alipata ajali kwabahati mbaya wakati akijaribu kuokoa mpira na kukumbana na mchezaji mwenzake Dejan Lovren wote wakiwa katika harakati za kuokoa mpira langoni mwao na hivyo kugongana.
Karius aliendelea na mechi licha ya kupata mshituko wa mwili kabla ya kupelekwa kwaajili ya kuuchungaza mkono na ndipo walipogundua kulikuwa na muachano kati ya mfupa na mfupa.
Alikuwa anatarajiwa kupaa kwaajili ya kurudi England kwa ajili ya kufanyiwa vipimo zaidi kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari nchini humo.
Mkufunzi wa kikosi hicho Jurgen Klopp alikuwa anatarajiwa kumwanzisha katika mechi ya ufunguzi ya ligi dhidi ya Arsenal lakini Simon Mignolet raia wa Ubelgiji anaonekana kurudi kwenye nafasi yake.
Lakinipia zaidi ya Mignolet, Liverpool wana golikipa wa zamani wa klabu ya Arsenal Alex Manninger aliyesajiliwa kwa usajili huru akitokea klabu ya Ausburg.
Post a Comment