SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: SEVILLA; Tunatoa Kitu, Tunaingiza Kitu.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ni kamsemo kanakojitokeza baada ya klabu ya Sevilla kumruhu Kevin Gameiro kutimkia klabu ya Atletico Madrid, na sasa wamemsainisha fow...






Ni kamsemo kanakojitokeza baada ya klabu ya Sevilla kumruhu Kevin Gameiro kutimkia klabu ya Atletico Madrid, na sasa wamemsainisha fowadi Wissam Ben Yedder kutoka nchini Ufaransa, klabu ya Toulouse kwa jumla ya miaka mitano.

Ben Yedder, 25, amesajiliwa kwa thamani ya euro 9mil baada ya kuifungia klabu yake ya zamani magoli 23 msimu uliopita na kuisaidia Tolouse kutokushuka daraja.

''Ben Yedder ni mchezaji mpya wa klabu ya Sevilla" imeandikwa hivyo katika ukurasa wao wa twitter.

Sevilla wamemuuza mfungaji wao bora wa msimu uliopita aliyetimkia klabu ya Atletico Madrid  na tayari uongozi wa klabu hiyo wameshajibu mapigo kwa kumleta mshambuliaji toka nchini Ufaransa Ben Yedder. Na hii ndio maana halisi ya toa kitu, leta kitu.

Mabingwa hao wa kombe la EUROPA mara tatu mfululizo, wanaonolewa na kocha Chilean Jorge Sampaoli baada ya kuondoka kwa Unai Emery kuelekea klabu ya PSG, pia amemleta Luciano Vietto kutoka klabu ya Atletica kwa mkopo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top