SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: David Moyes Kuchukua nafasi ya Big Sam.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
David Moyes ametangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Sunderland. Moyes 53, aliwahi kuzifundisha timu kama vile Everton pamoj...

David Moyes ametangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Sunderland.
Moyes 53, aliwahi kuzifundisha timu kama vile Everton pamoja na Manchester United, amekubali kibarua hicho kwamkataba wa miaka minne kwa kipindi chote atakachokuwa hapo Light stadium.
‘‘Nimekubali kuichukua klabu kubwa hapa England, na sapoti kubwa toka kwa wadau wangu, na ninachokitazama sasa, kurudi upya tena nchini England kwa ajili ya kufanya kazi.” Alisema Moyes.
Moyes raia wa Scotland, amekuwa nje tangu alipotimuliwa na klabu ya Real Sociadad ya nchini Hispania mwezi Novemba.
Moyes amekuja kuziba Pengo la Big Sam aliyekuwa kocha mkuu wa Sunderland, aliyetangazwa rasmi kuwa kocha wa England, kufuatia kujiuzulu kwa Roy Hogson baada mashindano ya EURO yaliyomalizika julai.
Mwenyekiti mkuu wa klabu ya Sonderland, Ellis Short amesema, hata hivyo Moyes alikuwa kwenye mipango yake muda mrefu sana wa kuwa kocha wa paka weusi, Sunderland.
‘‘Ni mtu ambae historia yake ya mpira inajieleza na ni mtu ambae muda mwingi nimekuwa nikitamani awe klabuni hapa”alisema Short. ‘‘Nimezungumza naye mambo kadha wa kadha, na nimevutiwa sana naye” alimalizia Short.
Moyes alianza kariya yake kama kocha na klabu ya Preston huko kaskazini mwisho na alikwisha wahi kupigiwa kura mara tatu kwenye tuzo za kocha bora miaka kumi na moja kabla ya kutimuliwa na klabu ya Everton.
Alichukua nafasi ya Mscotish mwenzake, Sir Alex Ferguson, aliyeiongoza klabu ya Manchester United kwa jumla ya miaka 26 kwa mafanikio makubwa.
Lakini licha ya kusaini kandarasi ya miaka 6 ndani ya Traford, alifukuzwa baada ya miezi kumi kwa kuipelekea timu kutokuwa na mataji na hivyo kutimkia Real Sociadad ya nchini Hispania kumpisha aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis Van Gaal.
Moyes alikuwa anahusishwa kuifundisha klabu ya Aston villa iliyoshuka daraja nsimu uliopita, lakini akajitoa mwenyewe kwa kuwatosa na nafasi hiyo kuchukuliwa na Dimatheo.
‘‘Ninachokitazama kwa sasa, ni kufanya kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na BIGSAM” Alisema Moyes.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top