SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Chris Coleman Ahusishwa Kujiunga Na Hull.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kocha wa sasa wa timu ya taifa ya WALES Chris Coleman, amehusishwa kujiunga na klabu ya Hull city inayoshiriki ligi kuu ya England. Mp...
Chris Coleman



Kocha wa sasa wa timu ya taifa ya WALES Chris Coleman, amehusishwa kujiunga na klabu ya Hull city inayoshiriki ligi kuu ya England.

Mpaka sasa Hull city hawana kocha baada ya aliyekuwa kocha wao Steve Bruce kuacha kibarua hicho kwa kutokuwa na mahusiano mazuri na makamo mwenyekiti wa klabu hiyo Ehab Allam.

Chris Coleman, 46 aliiongoza timu ya taifa ya Wales mpaka hatua ya nusu fainali ya mashindano ya EURO walipokubali kichapo cha magoli 2-0 dhidi ya mabingwa wa kombe hilo timu ya taifa ya Ureno.

Japo shirikisho la mpira wa miguu la nchini Wales limekataa kuwepo kwa mazungumzo na mabosi wa klabu hiyo, lakini tayari imekwishathibitishwa na huenda mabosi wa klabu hiyo wakapeleka ombi hilo juu ya kutaka kandarasi ya Coleman.

Mkataba wake ulikuwa uishe baada ya michuano ya EURO ya mwaka huu, lakini shirikisho la mpira limeona ni vema kuweza kumuongeza mkataba utakaomfanya Coleman kuendelea kuifundisha Wales mpaka mwaka 2018 na ataiongoza pia Wales kwenye kombe la dunia la mwaka 2018 litakalofanyika nchini Urusi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top