
Kocha mpya wa klabu ya Chelsea, Mwitaliano, Antonio Conte amesema, raia wa Colombia, Juan Cuadrado ni sehemu ya malengo yake akiwa klabuni hapo.
Juan Cuadrado, 28, aliyeshine akiwa katika ligi ya Serie A ya Italia, lakini pia katika kombe la dunia mwaka 2014, kabla ya kujiunga na klabu ya chelsea kwa pauni 23.3mil mwezi february mwaka 2015, alishindwa kufanya vyema katika mechi 13 alizocheza.
Cuadrado alipelekwa juventus kwa mkopo kwenye msimu wa mwisho na kuifungia timu yake magoli manne katika mechi 28 na kuisaidia klabu ya Italia kuchukua kombe la ligi ikiwa ni mara mbili mfululizo.
''Nilimhitaji sana kipindi nilipokuwa kocha wa Juventus, naamini atarejea katika makali yake ya zamani na kuweza kuisaidia klabu yake" Alisema Conte. ''sasa ni mcheaji wa Chelsea na tunaamini atakuwa nasisi na kama kuna mabadiliko yeyote, tutayaweka wazi" alimalizia Conte.
Akiwa anacheza nafasi muhimu, akiwa na msimu bora na klabu ya Juve, aliweza pia kuisaidia timu yake ya taifa kufika hatua ya tatu ya kombe la Copa America kombe lililochukuliwa na Argentina kwa mara ya pili mfululizo.
Post a Comment