
Kuelekea
mchezo wao wa kwanza wa CAF Confederations Cup 2016, mabingwa wa Tanzania
walijitahidi kufanya kila jitihada kuhakika wanapata kambi bora yenye utulivu,
na walitua Bejaia, Algeria wakitokea nchini Uturuki walikoweka kambi ya wiki
moja.
Mashabiki
wengi wa Yanga waliamini timu yao itapata ushindi kulingana na wapinzani wao MO
Bejaia kutokuwa na uzoefu mkubwa katika michuano ya vilabu barani Afrika, hata
mimi niliamini kikosi cha M-holland, Hans Van der Pluijm kingepata ushindi wake
wa kwanza dhidi ya timu za Kiarabu ugenini.
Kikosi
ambacho Hans alikianzisha tayari kilikuwa katika mawazo yangu siku moja kabla.
Niliamini timu itashambulia kwa kuwategemea Oscar Joshua katika beki 3 na Mbuyu
Twite katika beki namba 2.
Niliamini
Deo Dida atalindwa vizuri na Kelvin Yondan na Vicent Bossou na safu hii ya
ulinzi licha ya kuruhusu goli lililotokana na shambulizi la haraka lililokamika
dakika ya 20′, kwa pamoja watano hawa walifanya kazi nzuri katika ulinzi.
Thaban
Kamusoko na Haruna Niyonzima walijitahidi kuilinda timu na kudhibiti mpira
ndani ya dakika 30′ za kwanza ambazo wenyeji walifanya mashambulizi mengi.
Viungo hao wa kati waligeuka ‘mwiba’ kipindi cha pili, lakini bao la mlinzi
Salhi Yassine liliwaongezea nidhamu zaidi ya kujilinda MO Bejaia hasa wakitambua
TP Mazembe ilikuwa imeshinda 3-1 katika mchezo wa mapema wa kundi A.
Kiujumla
timu ilizidiwa sana dakika 25 za kipindi cha kwanza lakini uwezo mdogo wa
kimbinu wa Bejaia uliwafanya Yanga kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa goli 1-0,
matokeo ambayo yalisimama hadi mwisho licha ya jitihada kubwa za Deus Kaseke,
Amis Tambwe, Donald Ndombo Ngoma na Saimon Msuva.
Timu
ambayo ilifunga magoli manne dhidi ya Al Ahly na Esperanca imeshindwa kufanya
hivyo katika mazingira ambayo si rahisi kuamini, ila ndiyo ‘mpira wa miguu.’
MAMBO
MAKUBWA MAWILI YAMECHANGIA…
Yanga
kupoteza mchezo wake wa kwanza usiku wa kuamkia leo. Baada ya jitihada zote
kuhakikisha wachezaji na benchi la ufundi wanafanya maandalizi yao kwa uhakika,
uhuru na usalama, uongozi ulipatia kuipeleka timu Uturuki lakini ni wao
walioiangusha timu.
Kitendo
cha kuingia madukani kununua jezi mpya za kutumia katika mechi dhidi ya Bejaia
ni dalili za utendaji mbovu. Hapa napatwa na mshangao kiasi kwa maana CAF
waliwakataza Yanga kutumia jezi zao zilizozoeleka zikiwa na nembo ya mdhamini
wao ‘Bia ya Kilimanjaro’ kifuani.
CAF
wanasema klabu hazitakiwi kuweka chata za wadhamini wao sehemu kubwa ya wazi
katika jezi, kwa mujibu wa kanuni zao lakini ni ukiritimba tu wa kanuni mbovu
katika michuano mingi ndani ya Afrika. Yaani, mdhamini ambaye amenisaidia
kufika hapo nilipo, anakataliwa na kanuni tu wakati malengo makubwa ya
wadhamini ni kujitangaza na kutangaza biashara yao.
Kama
wangesema sababu za kiimani sawa, wangeeleweka ila hivi si haki kwa wadhamini.
Nawalaumu Yanga kwa kushindwa kuhudhuria semina elekezi ambayo CAF waliifanya
kwa vilabu vyote 8 vilivyofuzu kwa hatua hiyo ya makundi.
Kama TP
Mazembe wanahudhuria katika semina, Yanga pia walipaswa kufanya hivyo. Kwanza
kwa ugeni wao, pia wangejua mapema ni jezi za namna gani zinatakiwa kutumiwa na
klabu.
Kwenda
Uturuki, kujiita wa Kimataifa, mabadiliko ya ghafla ya jezi za kutumia na
kushindwa kuhudhuria semina elekezi ya CAF ambayo walitumiwa barua ya mwaliko
ni kielelezo tosha kuwa hawa nao ni, ‘Wakimataifa wanaoishi katika fikra za
mchangani…’
Kitendo
tu cha kuambiwa ubadilishe jezi katika ‘Ndondo’ ikitokea kufanana kwa jezi za
timu zote, huwa panachimbika.
Kwa
nini? Ni kwa sababu katika fikra zetu Waafrika tunaamini ni mkosi, na
kubadilisha jezi inachukuliwa ‘siriasi’ kama sababu ya kushindwa mchezo hata
kabla ya kuanza kwa mchezo. Mambo kama haya yanashusha morali ya wachezaji na
wakati mwingine yanavuruga saikolojia ya mchezaji kwa kufikiria sababu ya
kutokea kwa yote hayo.
Kitendo
cha CAF kuwazuia wachezaji wao wapya kucheza game ya jana usiku ni kielelezo
kingine kuwa uongozi unapaswa kuamka zaidi. Walikosaje kuzungumza na Simba SC
kirafiki na kuwaomba barua ya kumruhusu Hassan Kessy?
Kwa
namna alivyocheza Mbuyu-alilinda vizuri lakini hakuwa bora katika mashambulizi,
Kessy angecheza vizuri zaidi ya Mnyarwanda huyu. Juma Mahadhi kuna wakati Yanga
ilikuwa ikimuhitaji mchezaji kama yeye ili wapate goli lakini naye akapigwa
stop.
Kuwakosa
Mahadhi na Kessy dakika za mwisho naamini kulivuruga mbinu za mwalimu Hans
lakini hataweza kusema. Umakini mdogo wa uongozi au pengine uzoefu wao mdogo
kimataifa ndiyo sababu ya kuanguka kwa Yanga mbele ya MO Bejaia. Safari bado
inaendelea ila tujifunze kutokana na makosa yetu wenyewe. ‘Bora Kuliko’ inakuja
Dar es Salaam.
Ni
wakati wa Jerry Murro kufanya kazi yake vizuri na si kuchekesha watu kila mara.
Murro anapaswa kupita pita katika mitandao ya wapinzani wao, CAF atapata
faida ya kuisaidia zaidi timu yake. Hans pekee na benchi lake la ufundi
hawatoshi
Chanzo: Shafiidauda
Post a Comment