SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: BALE aiongoza vyema WALES
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
        WALES WAIBUKA KIFUA MBELE. na Charles kunji Wales ilijifurukuta na kuilaza Urusi mabao matatu kwa nunge katika mechi ya mwish...
        WALES WAIBUKA KIFUA MBELE.
na Charles kunji
Wales ilijifurukuta na kuilaza Urusi mabao matatu kwa nunge katika mechi ya mwisho na muhimu ya makundi jana usiku.
Aaron Ramsey na Neil Taylor na Gareth Bale walifunga mabao hayo muhimu na kuisaidia timu hiyo ya kocha Chris Coleman ikiwa imejihakikishia nafasi katika mkumbo wa pili kwa mara ya pili katika historia yake.
Wales kwa mara ya mwisho kufuzu mashibdano ya ulaya ilikuwa ni mwaka 1958 na tangu hapo wamekuwa hawana msimu mzuri katika mashindano kadha wa kadha ya ulaya.
Amani iliwajaa tele na nyuso za furaha tangu walipomwajili CHRIS COLEMAN alipoweza kuongoza timu hiyo ya wales kufuzu kwenye kombe la mataifa ya ulaya.
Wales wpo kundi B ambalo linazihusisha timu za England, Slovakia, urusi pamoja na wao wales.wakati wales walipoweza kumaliza mechi zao tatu katika kundi B kwa kuongoza kundi hilo kwa jumla ya pointi 7 wakiwa wameshinda mechi mbili na kupoteza mechi moja.dhidi ya England.
Msambuliaji wa kimataifa Gareth Bale aliiongoza timu hiyo katika ushindi wa magoli matatu kwa sifuri nay eye akikwamisha mpira mmoja wavuni na kumfanya mchezaji aliye na magoli mengi kwa sasa katika mashindano.

Bale anakuwa mchezaji wa kwanza kwa wales kufunga mechi tatu mfululizo kwa takribani miaka kumi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top