JULIO NA MPANGO WA KUISAIDIA TAIFA STARS.

Kocha wa timu ya Mwadui FC Jamhuri Kihwelo "Julio" amesema hana mpango wa kusajili wachezaji kutoka nje ya Tanzania kwenye kikosi chake cha msimu ujao
Julio amesema, lengo lake ni kutaka kutoa nafasi kwa wachezaji wazawa kuonyesha uwezo wao ili kuisaidia timu ya Taifa ambayo imekuwa haifanyi vizuri kutokana na kukosa wachezaji wenye viwango vizuri.
"Mipango yangu ni kutafuta wachezaji wa humuhumu ndani ya Tanzania kwa sababu kuna wachezaji wazuri lakini hawapati nafasi, mipango yangu ni kuvipandisha viwango vyao ili waje kuwa msaada kwa timu ya Taifa maana leo tunaona mfungaji bora wa ligi ya Vodacom wa kwanza hadi wa tatu wote kutoka nje," amesema Julio.
Kocha huyo ametamba kikosi chake kitafanya vizuri zaidi kwenye ligi ya msimu ujao huku akiwa na matumaini ya kumrudisha mshambuliaji wake Poul Nonga ambaye anataka kuondoka Yanga.
Post a Comment