![]() |
Picha na goal.com |
Uingereza walilazimishwa
sare ya uzembe na Urusi katika mechi ya awali, sasa wanalazimika kushinda
dhihdi ya Wales ili kujiweka katika mazingira mazuri
Adam
Lallana amesisitiza kuwa Uingereza watakuwa wajinga wa mwisho iwapo wataelekeza
nguvu zao zote kumkaba Gareth Bale watakapoikabili Wales katika mechi ya Euro
2016 Alhamisi.
Wales
wanaweza kutinga hatua ya mtoano kama watashinda mechi nyingine, na nafasi yao
kusonga mbele ni kubwa zaidi kwa kumtegemea supastaa wa Real Madrid Gareth
Bale.
Hata
hivyo Lallana ameelezea ubora wa kikosi cha Chris Coleman na amesisitiza kuwa
umakini unahitajika katika mechi ya Alhamisi.
'Wales
wana wachezaji wengi wenye vipaji kwa hiyo si Gareth Bale pekee wakuchungwa,'
fowadi huyo wa Liverpool alisema.
'Joe
Allen alikuwa nyota wa mchezo siku ambayo Wales walishinda dhidi ya Slovakia,
na hali kadhalika Aaron Ramsey.
'Ni
moja ya wachezaji bora watano duniani kwa sasa? Naam. Ni rafiki yangu sana na
mchezaji mzuri sana ambaye sote tunamfahamu. Lakini hatutamchunga Bale
pekee, huo utakuwa ni ujinga.
'Sisi
tunajitazama wenyewe, hatuna budi kuheshimu uimara wa Wales na kuchunguza
madhaifu yao, lakini kama tukicheza kwa kujituma tutaweza kushinda kila
mchezo.'
Katika
mechi ya Alhamisi meneja Roy Hodgson anafikiria kumuingiza dimbani Daniel
Sturridge.
Chanzo ni www.goal.com
Post a Comment