MAKALA YA EURO.
Na Charles Kunji.
![]() |
picha na bbc swahili |
Takribani miaka 56
tangu kuanzishwa kwa mashindano ya mataifa huru ya ulaya yakifahamika kama UEFA
EUROPEAN NATIONS CUP. Kwa mara ya kwanza mashindano haya kushika kasi ilikuwa
ni mwaka 1960, ambapo kuanzia hapo hadi sasa yameweza kufanyika mara 14 na mataifa
yaliyoweza kunyanyua kwapa kuchukua kombe hilo ni mataifa tisa pekee. Mataifa
hayo ni pamoja na ujerumani na Hispania
wote wakiwa wamechukua mara tatu. Ufaransa ambao ni wenyenyi wa mashindano ya
mwaka huu wao wameweza kunyanyua kwapa mara mbili, mwaka 1984 na mwaka 2000
wakichagizwa na ule moto wa mwaka 1998 walipoweza kumfunga brazil 3-1 kwenye
fainali ya kombe la dunia. Mataifa mengine ni soviet union [Russia], Italy,
jamhuri ya cheki, uholanzi, Denmark pamoja na ugiriki ambao wote kwa pamoja wamechukua
kombe hili mara moja. Kumbukumbu inatuambia kuwa, tangu kuanzishwa kwa
mashindano haya, ni mataifa matatu pekee ambayo ni Hispania, italia pamoja na
wenyeji wa mwaka huu ufaransa ndio wameweza kuchukua kombe hili katika ardhi ya
nyumbani. Msimu wa pili wa mashindano haya ambao ni 1964, Hispania ndiye
aliyekuwa mwenyeji na kuweza kuchukua kombe hilo. Waswahili wanasema jifunze furaha ya jirani
yako. Ndipo mashindano yaliyofuata katika mwaka 1968, italia akawa mwenyeji wa
mashindano na kuweza kufanya kama wlivyofanya Hispania katika miaka minne
iliyopita kwa kipindi hicho. Miaka 16 baadae, ufaransa akapata tiketi ya
kuandaa mashindano na kuweza kuitumia vyema nafasi ya kucheza nyumbani na
kuchukua kombe hilo. Nimiaka kadhaa sasa yapata umri wa wazee wetu hakuna tena
taifa lililoweza kuthubutu kufanya kama walivofanya Hispania, italia pamoja na
ufaransa.
Ni Hispania pekee ambao
wameweza kuchukua kombe hili kwa misimu miwili mfululizo. Waliweza kufanya
hivyo mwaka 2008 wakati wenyeji walikuwa ni AUSTRIA pamoja na USWISI. Safari
haikuishia hapo, Hispania katika miaka hiyo walikuwa na kizazi bora kabisa kama
vile CAROSY PUYOL, INIESTA pamoja na XAVI na wengineo wengi wakiongozwa na
delbosk na kombe la dunia kufanyika
katika ardhi ya Africa kwa mara ya kwanza Hispania tena wakaonyesha ubora wao
kwa kuchukua tena kombe la dunia kwa goli bora kabisa la kiungo iniesta. Ubabe
wa delbosk uliendelea tena kwenye EURO ya mwaka 2012 iliyofanyika Poland pamoja
na Ukraine ambapo Hispania tena kuchukua kombe kwa kumfunga italia magoli manne
kwa 0.
Ufaransa mwaka huu
wamepewa nafasi hiyo ya kuwa mwenyeji wakiwa na wachezaji kama vile hogo
lrolis, mandanda, bless matuidi, ngolo kante aliyekuwa na msimu bora kabisa
kwenye ligi ya uingereza, pamoja na greezman huku wakimchukua kinda ANTONIAL
MARTIAL anayekipiga katika klabu ya mashetani wekundu, Manchester united huku
wakimwacha nje benzima ambae anaandamwa na skendo za nje ya uwanja. Ufaransa ambao wana kikosi kilichosheheni
majina sio makubwa katika anga la kimichezo lakini wachambuzi wa soka wanaipa
nafasi kubwa kwa ufaransa kufanya vizuri. Wakiwa kundi A wapo na Albania,
Romania na uswisi mataifa yote yakiwa hayajawahi kuchukua kombe hili la
EURO. Baada ya mechi zote za makundi,
tutakuwa tumefahamu hatma ya ufaransa. Siku si nyingi nasisi hatuchoki kusubiri
tuone watakachokifanya.
Mataifa mengine ambayo
watu hawayapi nafasi ya kufanya vizuri ni pamoja na ubelgiji, cratia, pamoja na
mabingwa watetezi Hispania huku wingereza wakipewa nafasi finyu sana ya kutwaa
ubingwa.
Niliyekuandalia Makala
hii ni mimi CHARLES KUNJI mlimani radio. Elimu kwanza.
Post a Comment