
AMA kweli usemi unaosema mbuyu ulianza kama mchicha hakika bado unaishi kwenye fikra
ya kila chochote chenye mwanzo hapa duniani.
Ni dhahiri ya kuwa vitu vikubwa havikuanza kama nyangumi wa
bahari alivyo, bali vilipita katika mambo mengi mpaka kuja kuzoeleka katika
vichwa vya watu.
Katika mchezo wa mpira wa miguu zaidi tunaangazia michuano ya
mataifa ya Africa inayotarajia kulindima pale nchni Gaboni kuanzia januari 14, ya
2017.
Michuano hii ambayo inahusisha bara la Africa inayojulikana kama AFCON,
ilianza mnamo mwaka 1957 ikizihusisha nchi tatu ambazo ni timu ya taifa ya
misri maarufu kama mapharao wa africa ,sudani pamoja na Ethiopia,
lakini kwa
nchi ya afrika ya kusini walishindwa kufuzu kwa sababu ya ubaguzi wa rangi
uliokuwa umekithiri kwenye taifa hilo.
Tangu mwaka 1968, AFCON ilianza kufanyika baada ya miaka miwili na
ndivyo ilivyo hadi leo.
Kufikia mwaka 1998, zilianza kuingia timu 16 japo Nigeria
walijitoa na hivyo kubaki timu 15 pekee kwenye mashindano ya mwaka huo.
Hadi leo, hakuna mabadiliko yaliyofanyika na hivyo timu hizo 16
hugawanywa kwenye makundi manne ambapo kila kundi hutoa timu mbili zinazofuzu
kucheza hatua ya robo fainali.
Japo hawajaonekana kwenye nyuso za mashabiki kwa miaka saba,
taifa la misri ama mafarao, ndio timu pekee inayoongoza kwa kutwaa kombe hilo mara
nyingi zaidi.
Mafarao wametwaa kombe hilo mara saba, huku wakiweka rekodi ya
kutwaa kombe hilo mara tatu mfululizo toka mwaka 2006, 2008, na 2010 na hapo
ndipo machafuko ya kisiasa yakawapoteza mafarao kwenye soka la ushindani.
Timu ya taifa ya Camerron, Simba wasiofugika pamoja na timu ya
taifa ya Ghana maarufu kama black stars, wao wamenyanua kwapa mara nne wakati
Nigeria wakitwaa kombe hilo mara tatu.
Siku nne zikiwa zimebaki, wananchi wa taifa la Gabon wanaachana
na utalii uliozoweleka wa ndani ya nchi na badala yake utalii huo unahamia
kwenye nyasi za viwanjani kwa ajili ya kuwashuhudia magwiji wa soka barani Africa
wakionyesha uwezo wao.
Kwa taifa la Gabon, kwao hawana swali, hasa pale watakapokuwa
wakiona aina Fulani ya nywele zikipepea ndani ya uwanja huku kazi yao ikiwa ni
moja tuu, kuliimba jina ya Pierre-Emerick
Aubameyang huku wakishinikiza kombe hilo libaki nyumbani.
Hii ni
zaidi ya vita, hapa Sadio Mane wa Senegal, kule kuna Riyad Mahrez, mchezaji
bora wa Africa. Na kwenye milingoti miwili wapo akina Denis Onyango ambao
wanaweza kuwa kikwazo kwa washambuliaji wa timu mbalimbali.

Ni timu 16 kuchuana vikali ndani ya ardhi ya Ally Bongo.
Post a Comment