SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: YANGA KUREJESHWA TENA SHAMBA LA BIBI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
picha na zubery. LIGI kuu Tanzania Bara,VPL, inatarajiwa kuendelea tena katikati ya wiki hii ambapo jumla ya mechi saba zinatarajiwa k...
picha na zubery.

LIGI kuu Tanzania Bara,VPL, inatarajiwa kuendelea tena katikati ya wiki hii ambapo jumla ya mechi saba zinatarajiwa kupigwa.

Kubwa zaidi ni mchezo wa Klabu ya Yanga watakaokipiga na timu ya Mtibwa Sugar ambapo mchezo huo umeruhusiwa kuchezeka katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa kanuni ya 6, kipengele cha kwanza, Young Africa wametambulisha uwanja wa Uhuru kama uwanja wao wa nyumbani kwa sasa baada ya kuleta maombi, shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, ambapo baada ya kuyafanyia tathmini kwa mujibu wa kanuni hiyo ya 6, kipengele cha 6, TFF imeridhia klabu hiyo kuutumia uwanja wa Uhuru kama uwanja wao wa nyumbani.

Mbali na mchezo huo, pia kutakuwa na michezo mingine ambapo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya City watawakaribisha vinara wa ligi hiyo, timu ya Simba, Majimaji watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar katika uwanja wa Majimaji, mjini Songea wakati JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Mabatini.

Stand United itawakaribisha Azam FC kwenye uwanja wa CCM kambarage, wakati watoto wa Rahim Zamunda watakuwa wageni wa Mwadui FC kwenye dimba la Mwadui Komplex. Mwanza Derby’ kati ya Mbao na Toto Africans itapigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo. Alhamisi Oktoba 13, 2016 Ruvu Shooting itacheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Mabatini.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top