
MLINZI wa kutumainiwa wa klabu ya Mbeya City, Hassan Mwasapili amewataka mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na hofu kwenye mchezo wao dhidi ya klabu ya Simba utakaopingwa kwenye dimba la kumbukumbu ya Sokoine siku ya Jumatano.
Akizungumza na mtandao wa Mbeyacityfc.com Mwasapili alisema hana presha yeyote ya mchezo huo kwani anaifahamu vizuri klabu ya Simba hasa ukizingatia ya kwamba mchezo huo utakuwa ni mchezo wa tano tangu Mbeya city imepanda daraja.
"Huu utakuwa mchezo wangu wa tano kucheza dhidi ya Simba, naifahamu vizuri na nafahamu nguvu yao iko wapi. Siwezi kusema mengi juu ya matokeo yao msimu huu, hakika wameanza vizuri lakini kuna jambo moja la muhimu, mechi zote walizoshinda, wamecheza nyumbani, jumatano hii, utakuwa wakati wao mgumu kutokana na kuwa ndio mchezo wao wa kwanza kucheza nje ya Dar" Alisema Mwasapili.
Aidha, Mwasapili aliendelea kufafanua ya kuwa, pointi nne kwenye michezo miwili iliyopita zilitosha kuhifadhi nguvu ya kukutana na Simba na hivyo kuwa na matumaini makubwa ya kuwa watafanya vyema.
Post a Comment