
SIKU chache zilizopita kumekuwa na uvumi juu ya uwezekano wa Nahodha wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England, Wayne Rooney kuendelea kuwepo kwa klabu hiyo ya Old Trafford.
Hata hivyo, mkufunzi wa klabu hiyo, Jose Mourinho amethibitha ya kuwa Roooney ataendelea kusalia kwenye klabu hiyo kwani bado ana mipango naye.
Roone, 31 amekuwa haanzi kwenye kikosi cha kwanza tangu kipigo cha watford cha 3-1 na amekosa pia mechi mbili akiugua majeraha.
"Hakuna tatizo lolote juu ya Rooney, lakini mmekuwa mnatengeneza stori kwa ajili ya kuuza magazeti yenu" Alisema kocha wa zamani wa Chelsea.
"Rooney ni mchezaji wa daraja la juu na ni mchezaji muhimu sana kwetu, haendi popote, tunampenda na yeye pia bado anatupenda, amekuwa hana furaha kwa sababu ya kukaa benchi na mbaya zaidi amekuwa anachukizwa kwa kuwa na majeraha ya hapa na pale" Alisema Mourinho.
Hata hivyo, Rooney anaoneka kurejea kwenye kikosi baada ya kuwa kwenye majeraha ambayo yalimweka mbali na kipigo cha 4-0 dhidi ya Chelsea na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mancity kwenye EFL.
Staa huyo yupo numa magoli manne dhidi ya Bobby Chariton ambaye ni mfungaji wa muda wote wa timu hiyo akiwa na magoli 249
Post a Comment