SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: MAAGIZO YA NAPE ALIPOTEMBELEA TFF.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
WAZIR wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Nape Nnauye leo September 10 amefanya ziara katika ofsi za shirikisho la mpira wa miguu nch...
img_0086


WAZIR wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Nape Nnauye leo September 10 amefanya ziara katika ofsi za shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF akiwa na lengo la kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo utendaji wa shirikisho hilo lenye dhamana ya kusimamia masuala yote ya mpira wa miguu nchini.

Nape ambae amekutana na rais wa shirikisho hilo pamoja na watumishi wengine, ametoa agizo la kutafutiwa utatuzi kwa masula ambayo yapo ndani ya uwezo wake.

Katika moja ya maagizo ambayo Nape aliyatolea ufafanuzi ni kama haya yafuatayo.

Ukaguzi wa kina TFF
Nilimwagiza Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo amtumie mdhibiti na mkaguzi wa mkuu wa serikali afanye ukaguzi wa kina wa rasilimali watu ili tujue ukweli wa mambo ili watanzania waujue halafu ytuondokane na mambo ambayo wakati mwingine hayana msingi.
Kwahiyo utafanyika ukaguzi mkubwa pengine ambao haujawahi kufanyika muda mrefu kuangalia rasilimali fedha na rasilimali watu kuangalia uwezo wa utendaji.
Mishahara ya watumishi
Nimekuwa nikitumiwa message nyingi na watumishi wakidai hawajalipwa mishahara.watumishi wadai wanakaa muda mrefu wakati mwingine miezi mitatu minne hawajalipwa mishahara, manung’uniko yamekuwa mengi.
Rushwa kwenye uchaguzi
Niliahidi kwamba tutasimamia uchaguzi ndani ya TFF uwe uchaguzi wa haki usiogubikwa na matendo ya rushwa ili tupate viongozi wafasi.
Kupitia kikao hiki, nawaagiza TAKUKURU kote waliko, wahakikishe uchaguzi unakuwa wa haki kwa dhibiti vitendo vya rushwa. Kumekuweko na malalamiko mengi sana, sasa kuanzia mikoani wahakikishe uchaguzi unakwenda kwa haki.
Tukikuta mla rushwa tumkamate bila kujali cheo chake wala anatoka wapi, kusiwepo visingizio.nadhani hapa pakibanwa vizuri tutapata viongozi wasafi ambao wameshinda kwa uwezo wao na si kwa pesa zao.
Mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji wa vilabu
Michakato inayoendelea Simba na Yanga na timu nyingine ya kubadilisha mifumo ya uendeshaji. Serikali tunaunga mkono mabadiliko na mijadala. Michakato hii lazima iongozwe isije ikafata shor-tcut, lazima iwe ya uwazi pasiwe na mambo yanayofichwafichwa lazima sheria zifuatwe. Katika hili serikali tutakuwa wakali kwasababu likikosewa litavuruga amani ya nchi.
Thamani ya vilavu hivi inaangaliwa kabla ya mtu hajajipangia bei ya kujinunulia, kujikodishia  au kumiliki? Serikali tuko tayari kushirikiana na vilabu kufanya tathmini ya vilabu kabla ya kufikia hatua ya kumilikishana.
Ni vizuri kujua hadhi ya waliokuwa na vilabu hivi kwa miaka yote, wapo wanachama, mashabiki na wapenzi, hadhi na haki zao katika mchakato huu inaangaliwa vipi?

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top