
BAADA ya kikosi cha timu ya Tanzania Taifa
Stars kipo nchini Nigeria tayari kwa kutupa karata yake ya mwisho ya AFCON,
beki wa klabu ya Yanga amejiengua kwenye idadi ya watu 18 watakaocheza mchezo
huo.
Taarifa
ambazo shirikisho la mpira wa miguu Tanzania linazo ni kwamba Yondani
anamatatizo ya kifamilia ambapo hajayaweka sawa hadi wakati timu hiyo inaondoka
kwenda Nigeria.
Kocha
mkuu wa Stars Charles Boniface Mkwasa amesikitishwa na kitendo hicho lakini TFF
itasubiri ripoti ya kocha huyo mara baada ya kurejea kutoka Nigeria.
“Amepigiwa
simu hakupokea, ametumiwa ujumbe mfupi wa maandishi lakini pia akatumiwa ujumbe
kwa mfumo wa whatsapp lakini hakujibu. Tukazungumza na viongozi wa Yanga Katibu
Mkuu Baraka Deus Dedit akatuambia Yondani hayupo kambini kwao na sababu ya
kutokuwepo ni kwamba ametoa taarifa kwamba anamatatizo ya kifamilia”, amesema
afisa habari wa TFF Alfred Lucas ambaye alizungumza na Mkwasa muda mfupi kabla
ya safari.
“Jambo
hilo limemsikitisha sana mwalimu (Charles Boniface Mkwasa)kwasababu ni mchezaji
ambaye alimtegemea, lakini sisi kwa upande wetu (TFF) tunasubiri ripoti
ya mwalimu ndipo tuweze kuzungumza jambo au kutenda jambo.”
Stars
imeondoka Dar ikiundwa na wachezaji 18 huku nahodha wake Mbwana Samatta
akitarajiwa kuungana na kikosi hicho nchini Nigeria.
Post a Comment