
SIKU chahche baada ya kampuni ya uchimbaji
madini ya ACACIA ya mjini Shinyanga kutangaza kusitisha kuidhamini klabu ya
Stand United, sasa kampuni hiyo imeibuka na kuweka hadharani sababu
zilizowapelekea kusitisha udahamini wao.
Ofisa
habari wa kampuni hiyo Necta Foya ametaja kuwa, mvutano wa viongozi katika
klabu hiyo ndiyo sababu kubwa iliyopelekea wao kuachana na Stand United.
“Mkataba
wetu ulikuwa wa miaka miwili, kila baada ya mwaka mmoja tunafanya evaluation,
kwahiyo wakati tunaevaluate kuna maeneo gani ambayohayakuwa sawa,
kuna vitu ambavyo vilikuwa havijafanyika ndani
ya mkataba lakini vilevile kuna suala la changamoto ambazo zilikuwepo kwenye
mambo ya uongozi”, Foya alikaririwa na Sports Extra ya Clouds FM.
“Kwahiyo
kutokana na masuala mbalimbali, sisi ACACIA tukaona ni vizuri tuwaache hawa
ndugu zetu wa Stand United kwasababu tumeshakaa nao na kuzungumza nao mara
nyingi tu kwahiyo sio kitu ambacho tumekifanya ghafla”
“Tumewasaidia
ili waweze kujisogeza kwa miezi mitatu wakati wanajipanga upya, tumewapa dola
za Marekani 60,000 kwa upande huo ni kwamba tumeweka wazi kabisa na kuna hela
nyingine ambazo tulikuwa tunatakiwa kulipa kama dola 27,000 ikiwa ni malipo ya
mishahara ya wachezaji”
Post a Comment