
KAMPUNI
itakayoingia mkataba na Yanga chini ya Mwenyekiti Yusuf Manji, itajenga uwanja
wa mazoezi wa klabu hiyo.
Mmoja wa wajumbe wa baraza la
wadhamini, Francis Kifukwe amethibitisha hilo kwa kusema, kampuni inayokodisha
Yanga, imekubali kujenga uwanja wa mazoezi.
“Kweli kila kitu kinakwenda vizuri
na baada ya muda fulani, klabu itafanya suala la kuingia makubaliano.
“Suala la uwanja ni kweli,
tumekubaliana kuwa lifanyiwe kazi na kampuni hiyo imekubali kujenga uwanja
ambao utakuwa sehemu nyingine. Mbali na pale Jangwani ambako sisi tunataka
kujenga uwanja wa kudumu.
“Tayari kampuni hiyo imetoa
mapendekezo yake, sisi pia tunataka kutoa ya kwetu na kukaa ili kumalizana
katika hili,” alisema Kifukwe.
Manji, aliwaomba wanachama wa Yanga
moja ya kampuni zake kuikodi nembo na timu ya Yanga kwa kipindi cha miaka 10,
jambo ambalo Wanayanga walilipitisha.
Post a Comment