
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Italia ambaye alitolewa
bure na klabu ya Liverpool ya England kwenda klabu ya Nice ya Ufaransa, Mario
Balotelli, amerudi kwenye headlines baada ya maisha magumu ndani ya Anfield na
AC Milan ya Italia alipokuwa anacheza kwa mkopo akitokea Liverpool.

Balotelli ambaye kajiunga na Nice akitolewa bure baada ya
vilabu kadhaa kutoonesha imani ya kumuamini staa huyo, amefanikiwa kupachika
magoli mawili katika ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Olympique Marsella katika
mchezo wake wa kwanza kwenye klabu hiyo inayoshiriki ligin kuu ya Ufaransa.
Balotelli alitumia dakika 7 za mwanzo kuiandikia Nice goli la
kwanza kwa mkwaju wa penati na dakika ya 78 alipachika goli la pili lilifanya
wawe sawa na Marsella waliokuwa tayari wamewafunga goli mbili.

Goli la tatu la Nice lililowapa point tatu na kuwafanya
wapande hadi nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Ufaransa kwa kufikisha
jumla ya point 10, lilifungwa na Wylan Cyprien dakika ya 88, wakati magoli ya
Marsella yalifungwa na Thauvin dakika ya 14 na Gomis kwa penati dakika ya 72.
Hata hivyo, Baloteli ametanabaisha kuwa uamuzi aliouchukua wa
kujiunga na klabu ya Liverpool haukuwa uamuzi sahihi kwake na ndio maana hakuwa
na furaha licha ya kushinda magoli 4 katika michezo 28 aliyocheza.
“Licha ya kuwa na mashabiki wazuri na wachezaji waliokuwa na ushirikiano
na mimi lakini kiukweli sikuipenda kabisa Liverpool. Baloteli alisema muda
mchache baada ya kuisha mchezo wake wa kwanza akiwa na klabu ya Nice na
kuifungia goli mbili.
Post a Comment