BINGWA wa VPL timu ya soka ya Yanga imeendelea na programu
zake za mazoezi kwaajili ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam
utakaopigwa kesho Jumatano katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaa.
Katika
mchezo huo, ambao ni maalum kwa ajili ya ufunguzi wa ligi ligi kuu, Yanga
inaenda kushuka dimbani, huku ikitarajiwa kuwakosa nyota wake kadhaa kutokana
na kusumbuliwa na majeraha yaliyotokana na michezo yao ya Kombe la Shirikisho.
Wachezaji
ambao wanatarajiwa kukosekana ni pamoja na Ally Mustafa ‘Barthez’
anayesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu (ankle), mabeki Juma Abdul,
Andrew Vincent ‘Dante’ wanaosumbuliwa na maumivu ya miguu.
Wengine
ni Kevin Patrick Yondani anayesumbuliwa na maumivu ya jicho na kiungo
mshambuliaji Obrey Chirwa anayesumbuliwa na goti.
Mshambuliaji
tegemezi wa timu hiyo Mzimbabwe Donald Ngoma anarudi uwanjani baada ya
kukosekana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya MO Bejaia kutokana na
kuwa na kadi mbili za njano.
Yanga
ambao pia walikuwa wakisaka tiketi ya kufuzu nusu fainali ya Kombe la
Shirikisho Afrika, wametupwa nje baada ya Medeama kuifunga TP Mazembe goli 3-2,
kwenye mchezo uliopigwa nchini Ghana juzi.
Post a Comment